Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.
Tangazo
la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na
limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa
wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya
kutungua ndege.Gazeti hilo lilisema wawili hao waliuawa mapema mwezi huu.
Waziri huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un.
SOURCE: BBC SWAHILI