Pia, jumuiya hiyo imesema ipo mbioni kuanzisha hati ya maombi maalumu kwa Rais Kikwete (Petition Form) itakayosainiwa na mamilioni ya watanzania kumuomba Rais apuuze maazimio hayo ya bunge.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, kwa niaba ya jumuiya hiyo, Kaimu Mratibu wa jumuiya hiyo, Shaibu Sufiani alisema wameamua kufanya hivyo ili kuungana dhidi ya mabepari na madalali wa rasilimali za nchi.
Alisema jumuiya hiyo inaundwa na vijana wasomi wa vyuo vikuu nchini na nje ya nchi, ambapo amedai wana wajibu chanya kuhakikisha Tanzania inaendeshwa kwa kufuata misingi imara ya ukweli, uwazi, uwajibikaji.
“Tunapaswa kuzingatia msingi mkuu wa haki kwa kila mtu na watanzania waelewe kuwa kujiuzuru sio ushujaa au uzalendo. Jiulize wote waliojiudhuru hadi sasa ni wazalendo wa kweli wa nchi yetu?,’’alisema Sufiani.
Sufiani alisema panapotokea masuala yote ya kitaifa, masuala yanayohusu kuwajibishana, kutuhumiana, kushughulikiana kama wengine wanavyosema, basi lazima misingi yote iende sambamba na haki kwa kila mtuhumiwa.
Kwa mujibu wa Kaimu Mratibu huyo, alisema sote tunakumbuka kwamba Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekabidhi ripoti ya uchunguzi kuhusiana na sakata la TEGETA ESCROW.
Alisema msingi mkuu wa sakata hilo, unahusiana na kampuni ya kufua umeme ya IPTL, ambapo CAG kwenye uchunguzi wake iliarifu juu ya hadidu za rejea zaidi ya 11 iliyopewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Bunge na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
“Kwa nyakati tofauti, na kwa namna tofauti, sisi wenyewe, tumeshuhudia ripoti hiyo, na tumestahajabishwa na kugeuzwageuzwa kwa mapendekezo ya ripoti hiyo kulikofanywa na kamati ya bunge ya PAC,’’alisema.
Sufiani alisema ripoti ya CAG pamoja na viambatanisho vyake vyote, tumesoma na kuvirudia mara kwa mara hakuna sehemu, ambayo mkaguzi ameshauri, ama kupendekeza, ama kutafsiri kwamba pesa iliyokuwepo katika akaunti hiyo ni mali ya UMMA.
Pia, alisema katika ripoti ya CAG, hakuna sehemu hata moja au kurasa iliyosema kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amelisababishia hasara Taifa au Waziri au Katibu wa Nishati na Madini.
“Ripoti ya CAG hakuna sehemu yoyote inayosema kwamba fedha iliyotolewa kwenye akaunti ya ESCROW ni ama bilioni 321 au bilioni 306 kama wanavyouaminisha umma. Tunatambua mtachelewa kutuelewa, na mtashangaa kwa nini tumeamua kusema haya, lakini ni lazima tubadili sasa mfumo wetu wa siasa za Tanzania na siasa za kutatua matatizo na changamoto kama ilivyo sasa,’’alisema.
Sufiani alisema wanasiasa hasa wabunge, wamekuwa wakifanya maamuzi kishabiki, kichuki, kimaslahi binafsi na bila kuzingatia ukweli na misingi ya utawala bora huku ripoti ya CAG ikisema wazi imefanya jitihada stahili kuhakikisha taratibu zinafuatwa ili kujiondoa kwenye madhara yanayoweza kutokea baada ya fedha kutoka.
“Ripoti ya CAG haijamtia hatiani mtu yeyote. Tunashindwa kuelewa misingi ya Kamati ya PAC ya kutaka kuwajibishwa kwa watu bila ya kuwa na hatia.
vyovyote itakavyokuwa, na vyovyote itakavyotafsiriwa, imetoka wapi?,’’alisema.
Sufiani alisema kuwapoteza watu kama Waziri wa Pro.MUHONGO, kwenye utumishi wa umma, kwa sababu tu Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hana mahusiano mazuri na madalali wa rasilimali za nchi hii, ambao historia imeonyesha maeneo kadhaa walipoiaminiwa na kuharibu.
Alisema pia, kumpoteza Profesa Muhongo kwa sababu tu tangu kuingia kwake ofisini ameziba mianya ya uchotwaji mkubwa wa fedha za watanzania kupitia sekta ya madini, na sasa mabepari wameungana na wabunge wenye husuda kupambana dhidi ya ukweli na haki anayosimamia Waziri.
“Kumpoteza Muhongo kwa sababu tu yeye na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi, hawana mawasiliano mazuri na baadhi ya wabunge au wajumbe wa PAC juu ya kitendo chao kudhibiti udalali wa rasilimali,’’alisema
Sufiani alisema watanzania wanapaswa kujiuliza maswali, ambayo PAC wanapaswa kutujibu ikiwemo kutueleza, ni katika ukurasa wa ngapi, aya ya ngapi, nukta ya ngapi iliyopo kwenye ripoti ya CAG inayosema kwamba ESCROW ni MALI YA UMMA?.
Pia, alisema wanaitaka PAC iwaeleze, ni katika ukurusa wa ngapi, iliyopo kwenye ripoti ya CAG inayosema kwamba watendaji hao wa serikali wamefanya makosa na wanapaswa kuwajibisha.
“Tunaitaka PAC itueleze, kama kulikuwa na mchezo mchafu, na wakauthibitisha, iweje Wizara ya Fedha isihusike?, kwa nini Gavana wa BOT na timu yake na Waziri wa Fedha na timu yake nao wasihusike kwenye hilo kwa kuwa fedha ilikuwa kwao,” alisema.
Alisema kama kweli kulikuwa na mchezo mchafu, iweje BRELLA, na Wizara inayoisimamia ambayo ni viwanda na biashara na Waziri wake na timu nzima wasiwajibishwe nao kusajili kampuni ambayo wanadai siyo halali.
“Kama ni kweli kuna tatizo, iweje TRA wakubali kupokea kodi ya zaidi ya bilioni 30 kutoka kwa mbia wa IPTL ambao ni VIP iliyotokana na mauzo ya hisa 30% kwa PAP?. Kwa nini TRA isiwajibishwe kwa kupokea fedha haramu na kuziingiza kwenye mapato ya serikali ilihali ikijua ni fedha haramu?,”alisema.
Kutokana na hali hiyo, Sufiani alisema suala nzima la ESCROW limegubikwa na siasa, maslahi binafsi, chuki, wivu na kukomeshana, Hivyo tunamuomba Rais Kikwete asitekeleze azimio hata moja mpaka kwanza umma utakapoelewa ukweli halisi wa mbivu na mbichi na kila lililo nyuma ya pazia kuhusiana na sakata hilo.
“Tunamuomba Rais aunde chombo huru, ili suala hili lichunguzwe na kufanyiwa maamuzi huru ikiwemo na tuhuma za baadhi ya Wabunge kuhongwa, kununuliwa na kuwa mawakala wa Benki ya Standard Charterd,’’alisema.
Hivyo, alisema wanamuomba Rais, aviagize vyombo vyake vya ulinzi na usalama viwachunguze wabunge wote wanohusika kwa tuhuma kutumiwa, kuhongwa na kununuliwa ili kutuondolea watetezi wetu wa rasilimali.
1 comments:
I want to share my testimony of how i become rich and famous today… i was deeply strangled up by poverty and i had no body to help me, and also i search for help from different corners but to no avail… i see people around me getting rich but to me i was so ashamed of my self so i met a man on my way he was very rich and he was a doctor so he told me something and i think over it though out the day so the next day i looked up and i keep repeating what he said to me. ” if you want to get rich quick and be famous” you need to cross your heart and do what is in your mind so i tried all i could in other for me to do as he said so later on i told my fellow friend about this same thing then my friend was interested in my suggestions so i decided to look in the internet and i found their number so we decided to contact them and unfortunately we did as they instruct us to do and later they told us to get some requirements and all the rest… so this initiation took us just a week and later on the great fraternity gave us $1,200,000 to start up our lives…. and now am testifying that if in any case you want to join any great fraternity all you need to do is for you to contact them because they are legitimate and they do as what they instructed them to do, so you can as well WhatsApp: +233594515977 or you can Email: Markroland08011@gmail.com
EmoticonEmoticon