NA MWANDISHI WETU.
Kampuni ya IPTL/PAP imewataka wanasiasa kuzingatia ukweli
halisi kuhusiana na kampuni hiyo kuwa ni kampuni binafsi inayojishughulisha na
uzalishaji na uuzaji wa umeme na si
shirika la umma.
Pia, imesema kuendelea kujadili masuala ya ndani ya
uendeshaji ikiwemo namna ya kuuza na
kuzalisha umeme, umiliki na uhalali wa kampuni, uuzaji na ununuaji wa hisa za
kampuni ni masuala binafsi ya kampuni .
Taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari jana mjini Dar es saalam, Katibu na mshauri wa
sheria wa kampuni hiyo Joseph Makandega
ilisema IPTL/PAP ni wadau wa
kuzalisha na kuuza umeme kwa shirika la umeme
nchini(TANESCO).
Ilisema kinacho waunganisha IPTL na umma ni huduma wanayo
itoa kwa TANESCO ya uuzaji wa umeme, hivyo kulazimisha umma kujadili mambo ya IPTLya sasa na ya zamani
ni upuuzi unaopaswa kudharauliwa .
“Kulazimisha umma kujadili migogoro ya sasa nay a zamani
kama mgogoro wa Mechmar na VIP ni sawa na kuwalazimisha watu wajadili migogoro
mingine binafsi ya kampuni ambayo si ya umma,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza; “pia ni sawa na kulazimisha jamii fulani iache shughuli
zao na kujadili mambo bimafsi ya mtu, jambo ambalo si haki na ni upuuzi na
inapaswa kukemewa .
Ilisema kampuni binafsi na makini kama IPTL/PAP ina sera
zake na misingi yake ya uendeshwaji ,
hivyo kuruhusu hisia binafsi za wanasiasa uchwara kutawala mjadala kuhusu
uendeshwaji wa kampuni ni upuuzi wa kiwango kikubwa.
“Nawasihi wanasiasa hawa japo tunatambua ni wakina nani wanawatumia na kwa maslahi gani? kamwe
wasichokoze moto wasioweza na muda si mrefu tutaweka wazi uozo wao wote
,”ilisisitiza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Makandege ilisema inawashauri wanasiasa
waliokuwa mstari wa mbele kueleza uongo
juu ya IPTL/PAP kuwekeza nguvu zao
katika kutimiza ahadi zao walizozitoa kipindi cha uchaguzi ikiwemo kuinua
uchumi wa wananchi wanao waongoza.
Alisema miongoni mwa
wanasiasa hao viherehere wameshindwa kutimiza ahadi zao na sasa wanatafuta
umaarufu wakisiasa kupitia suala la IPTL
na kuaminisha umma kuwa mali yao wakati
sio kweli .
Hivyo, taarifa hiyo ilisema IPTL/PAP inajua ni namna gani
hisa za VIP walivyozinunua. Vilevile inafahamu namna hisa za Mechmar zilivyo
nunuliwa sisi ni wataalamu wa masuala ya biashara , uwekezaji, uzalishaji, na
viwanda hii si siasa wafanye siasa yao bila kuingilia masuala ya kitaalamu.
Kupoteza muda wa watanzania kuwajadilisha masuala binafsi tena kwa uongo wa
hali ya juu ni jambo ambalo halivumiliki kuwakalia kimya wanasiasa kwahivyo ni kuutumia vibaya muda wa
watanzania.
Makandege aliwakaribisha watanzania wote wanaotaka kufahamu
maswala mbalimbali yanayohusiana na IPTL/PAP ikiwemo umiliki na uzalishaji wa
umeme kutafuta taarifa sahihi kutoka
kwenye vyanzo sahihi ambavyo ni wao na
si wanasiasa.
Yapo masuala, taasisi na mashirika ambayo ni mali ya umma na
watanzania wanaona namna ambavyo yanafujwa na mengineyo yanafujwa na wanasiasa
haohao waliojivika usemaji wa IPTL,huku wakishinwa kuyatetea mashirika hayo na
badalka yake wamekuwa sehemu ya ufujaji na wanaifanya IPTL kama kivhwa cha
kujifichia tunaushahidi na vielelezo vyote na tutaweka wazi muda wowote ili
watanzania wawapime malaika hao kama ni malaika au mashetani.
SOURCE: GAZETI LA MAJIRA
7 comments
hii kweli kabisa hawa wakina kafulila hawaoni makampuni ya umma yanavyofujwa wao wameng'ang'ania kampuni binafsi,wanataka nini hawa au rushwa
Hivi hawa mbwa kina KAFULILA na ZITTO KABWE wanamtatizo gani mbwa hawa?? Wamekaa kama mademu mbwa hawa kazi kupika majungu tu wanashindwa kutekeleza ahadi walizozitoa majimboni kwao mbwa hawa wanabaki kufanya majungu mjini hapa!! wataliwa mbwa hawa
Hakuna haja ya kuwaficha hawa ni Mbunge DAVID KAFILILA na ZITTO KABWE. Wanasiasa uchwara hawa, wachumia tumbo. Kazi yao ni kutengeneza scandal ili wapate riziki.Kwa IPTL/PAP wamechemsha, watapiga kelele mpaka makoo yawakauke. Watanzania tumegundua hila zao.
n times like this haya mambo ya mascandal yatasikika sana as long as mwakani ni uchaguzi yatakuwa yaleyale kama 2010, leo tumepata wabunge wa scandal ya EPA/RICHMONDS walipita hivihivi baada ya watanzania kuhemka. Ndio leo tunao kina KAFULILA na wengineo, wameshindwa kutekeleza ahadi zao wamebaki kubeba fitna na migogoro ya kibiashara ya watu wengine.
Bongo kuna wanasiasa basi, wachumia tumbo tu hawa jamaa, nakumbuka KAFULILA na familia yake walivyo kuwa wakicheza ngoma yakwao pale bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge. Mpaka kichefuchefu
PAP/IPTL wapuuze hizi mbwembwe za wanasiasa wao waconcetrate kwenye kuhakikisha wanatugea umeme watanzania kama walivyoahidi kwenye mikataba yao
mpaka kielewekeeeeee!!!!
EmoticonEmoticon