IPTL/PAP YAMVAA KAFULILA


IPTL YATAKA WANANCHI WAMPUUZE









Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP), ambayo ni mmiliki halali wa kampuni ya
IPTL imempuuza, kumshangaa na kumdharau mbunge wa Kigoma Kusini-NCCR Mageuzi, David Kafulila kwa
taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari Oktoba 5, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu na Mshauri wa sheria IPTL/PAP, Joseph Makandege imesema
Kafulila anaweweseka na hii inatokana na umma kushindwa kukielewa anachokisimamia ndio maana
analazimisha masuala ya uongouongo yaaminiwe na umma.

Makandege alisema Kafulila anajua fika kwamba IPTL ni mali ya PAP, baada ya VIP na MECHMAR kuuza hisa
zao kwa PAP na hili jambo sio siri na limeripotiwa katika vyombo vyote vya habari Tanzania anaweza
akarejea taarifa ya aliyekuwa mmiliki wa VIP, James Rugemalira aliyeitoa Agosti 29, 2013.

Katika taarifa ya Rugemalira, Makandege alisema mmiliki huyo wa VIP alieleza namna ya mchakato wa
manunuzi ulivyokwenda baina ya PAP na VIP, hivyo Kafulila aache kuota ndoto za alinacha kwa kuwa kila
mwenye akili timamu anafahamu kwamba IPTL/PAP inauzia umeme TANESCO tangu mwaka 2002 na mwaka 2006,

VIP na MECHMAR iliingia katika mgogoro wa kimaslahi na kupelekea kusainiwa kwa makubaliano ya kisheria
ya ESCROW na hatimaye na kufunguliwa kwa akaunti ya ESCROW, ambayo BoT alikuwa wakala wa ESCROW na si
mmiliki wa fedha za ESCROW.

"Kafulila amefulia, hivi jiulize ukiwa wakala wa M Pesa au TIGO, unakuwa mmiliki wa M PESA au TIGO
PESA hiyo, Kwa hiyo BoT alikuwa wakala wa fedha za ESCROW na sio mmiliko wa fedha za ESCROW,''ilisema
taarifa hiyo.

Makandege alisema Kafulila anafahamu fika kuanzia tangu kusaniwa kwa makubaliano ya ESCROW Julai 5,
2006, TANESCO walikuwa wanaendelea kupatiwa umeme kila siku, kwa kiasi kilekile wanachokihitaji wao mpaka leo hii na anajua kwamba, TANESCO walikuwa hawailipi IPTL na badala yake fedha walikuwa wanaziweka katika akaunti ya ESCROW, Je Kafulila alitaka tuwape umeme bure TANESCO. Je yeye anapofanya kazi bungeni halipwi?, Anapokaa katika vikao vyake hapewi posho au wanaomtuma kueneza uongo
hawamlipi?. Kafulile aache kutumika vibaya.

"Dunia nzima inafahamu sasa kwamba PAP/IPTL imepewa dhamana ya kuzalisha megawati 2000 nchini Kenya na
hilo inathibitika katika barua kutoka serikali ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge Agosti 19, 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.,''ilisema.

Taarifa hiyo, ilieleza barua ya Kenya kumtaka Singasinga Seth azalishe umeme Kenya ilikuwa ina kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari ''Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania''.

Makandege alisema Kafulila anaposema Singasinga Seth haruhusiwi kufanya biashara Kenya, wakati Singasinga huyo huyo, ameshapewa kibali cha kuzalisha umeme na kuuza Kenya ikiwa ni mara 20 zaidi anayozalisha Tanzania, Hivyo ni kichaa pekee anayeweza kuamini upuuzi huu wa Kafulila.

''Tunapenda kuwasisitizia watanzania waendelee kumpuuza mtu huyu kwani kwa sasa amevurugwa ndio maana anahamishahamisha mijadala na kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri huku akijua ESCROW ni jambo la kisheria na si la kisiasa na yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya ESCROW hata kwa njia ya mtandao

ili siku nyingine asiendelee kulishwa ujinga wa namna hii bila kujua ukweli wa ndani kufanya hivyo ni kufedhehesha watanzania kwamba wanawachagua wabunge wenye uelewa mdogo kama Kafulila''. ilisema taarifa hiyo.

Ilisema uelewa finyu huu wa Kafulila unamsababisha ashindwe kutofautisha kati ya mali ya umma na mali binafsi, fedha za umma zilizopo BoT na uwakala wa ESCROW wa BoT, kazi za serikali na kazi za mbunge kazi za IPTL/PAP na kazi za TANESCO tunasisitiza IPTL/PAP sio shirika la Umma wala mali ya serikali,

Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.

Hivyo, tunawahakikishia watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu  na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh. 80 uko mbioni  kukamilika ili watanzania wafurahie huduma ya umeme na wachagize maendeleo yao japo kina Kafulila na  wapinzani wetu wa kibiashara hawapendi watanzania wafaidi matunda yao.

SOURCE: GAZETI LA MAJIRA 8th October 2014


EmoticonEmoticon