MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilisikiliza ushahidi wa
mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Hans Aingaya Macha akitoa
ushahidi katika kesi inayomkabili ya kughushi.
Macha alitoa ushahidi wake, wakati upande wa mshitakiwa unaoongozwa na
Wakili Deogratius Ringia mbele ya Hakimu Devotha Kisoka mahakama hapo
jana.
Mfanyabiashara huyo, alidai mahakamani hapo kuwa nyumba ya ghorofa tano
kilichopo katika kiwanja namba 183 ‘A’ kilichopo Kigogo, aliinunua kwa
Ramadhan Balenga huku akiwa pia anamdai Balenga.
Hata hivyo, Wakili wa serikali Nassoro Katuga alipomuuliza swali
mshitakiwa huyo aonyeshe ushahidi wake, ikiwemo nyaraka za madeni na
awataje majina ya mashahidi waliokuwepo wakati akinunua nyumba hiyo ya
ghorofa tano kwa sh. Milioni 20, alidai wapo.
Kitendo ambacho, kilimfanya mshitakiwa huyo kudai mahakamani hapo kwa
jina moja tu, ndipo aliwapowaambia awataje na yeye aliwataja akiwemo
mfanyakazi wa Balega aitwaye Mohammed Waziri.
Alipomaliza kutoa ushahidi wake, Macha, ndipo zamu ya Wazir ilifika,
ambaye alidai mahakamani hapo kuwa hakuwahi kushuhudia mauzo yeyote
yakifanyika kwa kuwa wakati huo alishaondolewa katika biashara alizokuwa
akizifanya.
“Sifahamu chochote kuhusiana na Balenga kuuza nyumba, ingawa niliambiwa
na watu wa pembeni, akiwemo Macha mwenyewe, hivyo huo ndio ukweli
wenyewe Mheshimiwa Hakimu ninaoujia,’’kauli ambayo iliamsha cheko katika
chumba cha mahakama kutokana na ushahidi wake huo.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa mke wa Balenga, Nully Ahmady alidai
mahakamani hapo kuwa hata yeye hakushuhudia wakati akiuza nyumba hiyo,
kwa kuwa alikuwa tayari ameshaachana naye. Kesi hiyo inaendelea tena
mahakamani hapo.
Picha: Mfanyabiashara Macha
SOURCE: Jamii Forums.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
EmoticonEmoticon