KAMPUNI YA MUGABE YAKABILIWA NA MASHTAKA
Kanisa la Reform linasema kuwa ardhi hiyo inamilikiwa na kundi la shule zake la Eaglesvale.
Wakili wa shule hiyo Rodney Makausi aliambia BBC kwamba mwaka 2016 serikali ilichukua ardhi hiyo kwa nguvu.
Serikali baadaye ikaondoa madai yake baada ya swala hilo kuwasilishwa mahakamani.
HABARI: BBC SWAHILI
Kagame azungumza na Donald Trump
Viongozi hao walikutana mjini Davos nchini Switzerland walipokuwa wamehudhuria mkutano ulioandaliwa na World Economic Forum.
Dawa za nguvu za kiume zawaponza Zambia
Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, ameiambia BBC kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili.
''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa''
Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hiko cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza bwana Kasolo.
Wanaume hao watatu wanatoka katika mji mdogo wa katete, na si wagonjwa wa kipindupindu bali walikunywa dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa inayojulikana kama Mvubwe.
Ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mwaka jana ulisababisha vifo vya watu takribani 70, kusini mwa Afrika.
Rais Edgar Lungu mwezi uliopita, alitoa agizo kwa jeshi la Zambia kusafisha maeneo ya masoko na kuondoa uchafu ambao ndio saabu ya kipindupindu.
Habari Mali ya BBC Swahili
Croatia yatoa kitabu cha hadithi cha watoto,kinachoonyesha wazazi wenye jinsia moja
Kwa mara ya kwanza Croatia, kitabu cha watoto cha hadithi za kusimulia kitandani Kimejumuisha wahusika ambao ni wapenzi wa jinsia moja. kinajumuisha msichana aliye na baba wawili, na mvulana aliye na mama wawili. Je, unadhani kitabu kama hicho kinafaa watoto? #