MCHANGE
NA KIBAHA TUITAKAYO
Mwanasiasa kijana aliyeteka mioyo ya vijana wa kibaha
mjini na wakazi wa kibaha kwa ujumla ambaye pia alikuwa mgombea wa ubunge
katika jimbo la kibaha mjini na kushika nafasi ya pili ametangaza kushiriki
mdahalo mkubwa ulioandaliwa na vijana wa Kibaha.
Mdahalo huo uliopewa jina la Mchange na Kibaha
Tunayoitaka umelenga mambo kadha wa kadha ikiwemo:
Mosi kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo hilo la
Kibaha Mjini ambalo ana nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kukubalika sana
wakazi wa jimbo hilo ambao wanasubiri kwa hamu kujua endapo atagombea ubunge
kwa jimbo lao au la?
Mchange ambaye pia aliwahi kuwa kada mkubwa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo,alipopigiwa simu kuthibitisha taarifa hizi alisema “naomba wananchi wa Kibaha wafike kwa wingi
ili wachambue pumba na mchele ili wafanye chaguo sahihi wakati wa uchaguzi,na
wasirudie makosa waliyofanya 2010”
Habibu Mchange aliendelea “Nimepewa heshima kubwa na Vijana wa jimbo langu na naahidi
sitawaangusha katika hili,na nashukuru kwa kuniunga mkono katika safari yangu
ya siasa”.
“Pia
ninashukuru wakina mama wote wa kibaha mjini ambao wamekuwa nyuma yangu
wakinisapoti kwa kipindi chote ambacho nimekuwa nikifanya siasa ndani ya mji wa
kibaha” aliongeza Mchange.
Mchange alisema bado hajapewa taarifa na vijana hao eneo
la kufanyia mdahalo lakini atatangaza mara atakapopewa jina la ukumbi na
waandaaji hao wa mdahalo lakini utafanyika siku ya jumapili ijayo.
Mchange amekaribisha vijana kutoka pande zote za mji na
mkoa wa Dar es salaam ili kuja na kusikiliza yale anayotaka kuwaambia wana
kibaha mjini.
Imeandikwa na Serena Magezi