MCHANGE KUWASHA MOTO KIBAHA JUMAPILI






MCHANGE NA KIBAHA TUITAKAYO
Mwanasiasa kijana aliyeteka mioyo ya vijana wa kibaha mjini na wakazi wa kibaha kwa ujumla ambaye pia alikuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la kibaha mjini na kushika nafasi ya pili ametangaza kushiriki mdahalo mkubwa ulioandaliwa na vijana wa Kibaha.
Mdahalo huo uliopewa jina la Mchange na Kibaha Tunayoitaka umelenga mambo kadha wa kadha ikiwemo:
Mosi kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo hilo la Kibaha Mjini ambalo ana nafasi kubwa ya kushinda kutokana na kukubalika sana wakazi wa jimbo hilo ambao wanasubiri kwa hamu kujua endapo atagombea ubunge kwa jimbo lao au la?
Mchange ambaye pia aliwahi kuwa kada mkubwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,alipopigiwa simu kuthibitisha taarifa hizi alisema “naomba wananchi wa Kibaha wafike kwa wingi ili wachambue pumba na mchele ili wafanye chaguo sahihi wakati wa uchaguzi,na wasirudie makosa waliyofanya 2010”
Habibu Mchange aliendelea “Nimepewa heshima kubwa na Vijana wa jimbo langu na naahidi sitawaangusha katika hili,na nashukuru kwa kuniunga mkono katika safari yangu ya siasa”.
“Pia ninashukuru wakina mama wote wa kibaha mjini ambao wamekuwa nyuma yangu wakinisapoti kwa kipindi chote ambacho nimekuwa nikifanya siasa ndani ya mji wa kibaha” aliongeza Mchange.
Mchange alisema bado hajapewa taarifa na vijana hao eneo la kufanyia mdahalo lakini atatangaza mara atakapopewa jina la ukumbi na waandaaji hao wa mdahalo lakini utafanyika siku ya jumapili ijayo.
Mchange amekaribisha vijana kutoka pande zote za mji na mkoa wa Dar es salaam ili kuja na kusikiliza yale anayotaka kuwaambia wana kibaha mjini.

Imeandikwa na Serena Magezi


EmoticonEmoticon