RADAR JNIA KUANZA KAZI DECEMBER 21




Kutoka: Gazeti la Jamvi la Habari
BAADA ya kukamilika ujenzi wa jengo la kufunga mfumo wa rada ya kisasa wa  kuongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataif wa Julius  Nyerere (JNIA), hatimaye mashine zimeanza kufungwa.
Ufungwaji wa rada hiyo, nimipango ya serikari ya awamu ya tano ambapo mradi huo, utahusisha viwanja vingine vitatu ambvyo ni Uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), Songwe na Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mhandisi Mshauri wa Miradi JNIA, Stephine Mwakasasa, alisema kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Desemba 21 mwaka huu.
Alisema, mara baada ya kufungwa mfumo huo, utaanza kazi  kwa majaribio, hata hivyo, alibainisha kuwa Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari ndiyo atatangaza rasmi siku ya ufunguzi wa mfumo huo na kuanza kazi.
“Kama mnavyoona kwamba kazi inaendelea vizuri tu, tunatarajia kumaliza kazi hii muda mfupi lakini kwa kuhusu kufunguliwa rasmi hilo watalizungumzia Watendaji wa TCAA,”alisema Mwakasasa.
Mwakasasa, alisema kukamilika kwa mfumo huo warada ya kisasa kutsidia kuongeza kampuni za ndenge kuja kutua katika uwanja huo kitendo ambacho kitaliongezea taifa mapato.
Naye Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATAA), Aristid Kanje, alisema chuo hicho kimezalisha wataalam wa kitanzania 7235 tangu kilipoanzishwa miaka 35 iliyopita.
Chuo hicho kilianzishwa mara baada ya kuvujika Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 tukio ambalo lilifanya Tanzania isiwe na chuo cha kufundishia wataalamu wake wa sekta ya Usafiri wa Anga.
Kanje, alisema kuanzishwa chuo hicho kumelisaidia taifa kupunguza gharama za kupeleka wataalamu wake kwenda kusoma nje ukilinganisha na awali wakati watanzia walipokuwa wakienda vyuo vya nje.
Alisema, miongoni mwa wahitimu hao, wanaume ni 6214 na wanawake 1021, ambao hivi sasa wameweza kulisadidia taifa katika kuleta mabdiliko ya kiutendaji katika sekta hiyo.
“Chuo lilianzishwa mwaka 1985 na hiyo ni baada ya ya kuvunjika Jumuiya ya Afrika Masharik mwaka 1977 kutokana mazingira hayo Tanzania ilibaki ikiwa haina chuo cha kufundishia wataalamu wake,”alisema Kanje.
Kanje, alisema chuo hicho kinatoa mafunzo kwa kiwango cha Kimataifa ambapo hivi sas kinadahili hata wageni ambao wanahudhuria mafunzo katika chuo hicho.
Aidha,Kanje alisema ili kuimarish ufafanisi katika chuo hicho,Serikali imenunua mtambo wa kisasa kwa ajili ya kufundishia, wenye thamani ya zaidi  Sh. Bili 1.
Pia alisema hivi sasa chuo hicho kina mpango wa kujenga chuo kikubwa cha kimataifa, ambapo uongozi uko katia mchakato wa hatua za mwisho kukamilisha adhima yake hiyo hususani kupata eneo maalum.
Kaimu Mkurugezi wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mbila Mdemu, alisema, serikali iliamua kuunda vyombo tendaji/Wakala mbalimbali zitakazokuwa zikitekeleza majukumu kwa uhuru lakini chini ya uangalizi wa karibu wa serikali.
Latest


EmoticonEmoticon