Chris Bomola
Tembo hao ni wa kutoka hifadhi ya Lwafi
Mwanamke wa miaka 60, ameuawa na tembo katika Wilaya ya Kalambo iliyoko Magharibi mwa Tanzania.Mashuhuda wa tukio hilo wanasema, tukio hilo lilitokea wakati marehemu akiwa anarejea kutoka shambani kwake majira ya saa nne asubuhi.
Hifadhi ya Lwafi inapatikana pembezoni mwa barabara ya kutoka Tanzania kuelekea Zambia.
Akithibitisha kutokea tukio hilo Mkuiu wa Wilaya ya kalambo Bi Julieth Binyura amewataka wananchi kuacha kuwafukuza tembo wanapoingia katika maeneo hayo badala yake kusubiri wataalamu kufanya kazi hiyo.
EmoticonEmoticon