Wizara ya mambo ya ndani nchini
Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya
kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda
nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake
Jana usiku
mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika
ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo
ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa
ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana
MigunaKatika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009.
"Kwa mantiki hiyo hati ya kusafiria ya Kenya ya bwana Miguna ilikuwa na bado ni batili", alifafanua bwana Njoka
Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baada ya kushiriki katika kiapo kisicho rasmi cha Raila Odinga kuwa rais wa watu wa Kenya mwezi uliopita.
CHANZO: BBC SWAHILI
EmoticonEmoticon