CCM mtawafukuza CCM Wazanzibar wangapi ??

Kila Mzanzibari alie CCM ambae ni kiongozi anaeonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM mwisho wake huwa mbaya na huvuliwa nyadhifa zote za uongozi na kutupwa kama mzoga na huonekana si lolote si chochote katika jamii ya wanaCCM.
Na hili zaidi hutendewa WaZanzibari tu ,angalia Akina Seif ;Ali HajI Pandu,na wenziwe wakati wa Nyerere walitimuliwa ,ni juzi tu Mansor Yousef nae katimuliwa ,hata haukujatulia kuna tetesi Mwanasheria Mkuu nae anaundiwa zengwe afukuzwe na nafasi yake apewe Jaji Mkusa Sepetu.
Mbona Tanganyika hakuna afukuzwae kuna mambo kibao ,hatusikii Mtanganyika kufukuzwa lile la Mwigulu kama angelisema Mzanzibar ndani ya bunge la Katiba ingelikuwa ameshapata la kumpata .
Mbali ya viongozi wakuu waliohusishwa na mambo mbalimbali ikiwemo rushwa na mikataba mibovu kama wangekuwa wazenji wangelikwisha fukuzwa chamani na kutolewa ndani ya Serikali .ila tunawaona akina Lowasa wavijisenti. wanapeta ndani ya CCM mbali waliojitangaza kugombea uraisi ndani ya CCM ,kama wangelikuwa wazenji basi wangekwishatimuliwa.
Sasa swala lakujiuliza jee ni nani alowapa jeuri hii na ujasiri huu Watanganyika ? Mimi naona sio bure kuna mkono wa wanafiki Wasaka Tonge(Wahafidhina Zanzibar).
Jee wao wamejisahau kua arubaini (40) zao ziko jikoni? Hii nikunyoyolewa mbawa kila Mzanzibar halisi na kuchomekwa Wazazibar ambao hivi sasa ndio wanao hodhi kila nafasi nyeti katika Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Ukenda Mahakamani Utaona wale Wazanzibar halisi walitimuliwa wote wakaekwa hao Mkuza Sepetu na Sasa anatayarishwa kuchukua nafasi ya Mwanasheria Othman Massoud, ukenda TRA ,ukenda Ma bank yote wamejaa yani Ukija Magreshen ndio wanapeana tu ndugu kwa ndugu waki Tanganyika.
Viongozi wetu wao namesake kulishwa maneno yakua Wazanzibar wako wengi Tanzania bara ? Lakini Chakujiuliza hao Wazanzibar waloko Tanzania Bara wengi si Wabangaizaji tu (Wafanya Biashara).
Lakini Zanzibar hakuna offisi hata moja unayokwenda kama hujaona Mkurigenzi ni Mtanganyika na Wasaidizi ndio Wazanzibar tukiachana na Wizara za Muungano ndio wanajikoga Wazanzibar hawana haki katika wizard hizo.
Ukiuliza Kwanini Wazanzibar hawa pewi nafasi katika wizard hizo za Muungano Wanasema Wazanzibar hawaja soma lakini , lakini hata hizo nafasi za Ufagizi na upikaji Chai huwa nautical huko huko Tanganyika, Jee sitahari hii kuvamiwa bila Kailua?.
Written by   //  07/09/2014


EmoticonEmoticon