Tatizo la mwanaume kupoteza au kukosa korodani

Kwa kawaida korodani hutengenezwa tumboni mwa mtoto upande wa mgongoni chini kidogo ya figo akiwa bado tumboni kwa mama, korodani hizi huanza kushuka taratibu pale mimba inapokuwa na umri wa wiki 35 hivi, hushuka kuelekea kiunoni na baadae nje ya mwili na kujihifadhi katika mfuko maalumu ya korodani iliyo chini au nyuma ya uume wake.
Ni tatizo au ugonjwa unaoweza kumpata mwanaume yeyote lakini zaidi kwa watoto wa kiume, hali hii inatokana na mtoto wa kiume kuzaliwa bila kuwa na korodani na hivyo mifuko ya korodani japo ipo lakini mitupu, au kuzaliwa na korodani lakini baadae zikapotea ghafla ukubwani.
Kupotea au kutokuwepo kwa korodani kunaweza kuhusisha korodani zotembili au moja, ni tatizo linalotokea kwa mtoto moja kati ya 100 wa kiume wanaozaliwa lakini huonekana zaidi kwa watoto waliozaliwa chini ya umri (hufahamika kama pre-mature au ndebile ) kwa takribani asilimia 4%.
Kwa kawaida korodani hutengenezwa tumboni mwa mtoto upande wa mgongoni chini kidogo ya figo akiwa bado tumboni kwa mama, korodani hizi huanza kushuka taratibu pale mimba inapokuwa na umri wa wiki 35 hivi, hushuka kuelekea kiunoni na baadae nje ya mwili na kujihifadhi katika mfuko maalumu ya korodani iliyo chini au nyuma ya uume wake.
Kordani zina kazi mbili, kutengeneza manii yaani mbegu za kiume za uzazi na pia kutoa homoni za kiume, kazi hiyo hufanywa katika joto la chini tofauti na lile la mwili kwa utofauti wa nyuzijoto 3 hadi 4. Joto kali huweza kuharibu korodani, ndiyo maana hushuka nje ya mwili.
Tatizo linalosababisha kutokuwepo kwa korodani kwa watoto ni pamoja na korodani kukosea njia ya kushuka wakati wa kushuka na hivyo kwenda sehemu nyingine katika kiuno au tumbo, njia ya kushukia kuharibika mfano kuwa finyu au kuziba, kuzaliwa chini ya umri n.k. Kwa mwanaume mtumzima au kijana ambaye awali alikuwa na korodani na ghafla zikapotea huweza kusababishwa na maambukizi katika korodani, joto kali kutokana na kuvaa nguo nyingi na nzito, ajali, kuumia katika michezo mfano mpira na hivyo kusaga korordani n.k.
Matibabu ya tatizo hili ni upasuaji pekee na si dawa, hakuna dawa ya kushusha au kuzirudisha korodani zaidi ya upasuaji.
source :mwananchi

EmoticonEmoticon