KAMPUNI YA MUGABE YAKABILIWA NA MASHTAKA


Kampuni moja ya rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe inatakiwa kuondoka katika kipade kimoja cha ardhi kinachomilikiwa na shule moja la sivyo ishtakiwe.
Kampuni hiyo kwa Jina Gushungu Holdings inadaiwa kunyakuwa kipande hicho cha ardhi chenye ukubwa wa hekari 23 katika eneo moja la makaazi ya mji wa Harare.
Kanisa la Reform linasema kuwa ardhi hiyo inamilikiwa na kundi la shule zake la Eaglesvale.
Wakili wa shule hiyo Rodney Makausi aliambia BBC kwamba mwaka 2016 serikali ilichukua ardhi hiyo kwa nguvu.
Serikali baadaye ikaondoa madai yake baada ya swala hilo kuwasilishwa mahakamani.
HABARI: BBC SWAHILI

Kigwangwala atembelea nyumba ya Baba wa Taifa-Magomeni

Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Hamis Kingwangwala amefanya ziara ya kutembelea nyumba ya Rais wa Kwanza na Baba wa Taifa Julius Nyerere, iliyopo magomeni jijini Dar es salaam. 
Picha kwa hisani ya Hamis Kingwagwala (twitter page) 

Rais Trump avishutumu vyombo vya Habari kwa kuandika habari Feki

Rais Donald Trump azungumza katika mkutano ulioandaliwa na World Economic Forum huku akivituhumu kuandika habari za uongo na kupotosha hotuba zake. 
Picture: Reuters

Kagame azungumza na Donald Trump

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Taifa la Marekani Donald Trump, ambapo wawili hao pamoja na mambo mbalimbali wamezungumzia mahusiano mazuri kati ya Marekani na mataifa ya Africa. 


Viongozi hao walikutana mjini Davos nchini Switzerland walipokuwa wamehudhuria mkutano ulioandaliwa na World Economic Forum. 

Tido Mhando Aburuzwa mahakamani

Mkurugenzi wa zamani TBC afikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara serikali.
Picha: citizen online

Dawa za nguvu za kiume zawaponza Zambia

Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, ameiambia BBC kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili.

''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa''

Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hiko cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza bwana Kasolo.

Wanaume hao watatu wanatoka katika mji mdogo wa katete, na si wagonjwa wa kipindupindu bali walikunywa dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa inayojulikana kama Mvubwe.

Ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mwaka jana ulisababisha vifo vya watu takribani 70, kusini mwa Afrika.

Rais Edgar Lungu mwezi uliopita, alitoa agizo kwa jeshi la Zambia kusafisha maeneo ya masoko na kuondoa uchafu ambao ndio saabu ya kipindupindu.


Habari Mali ya BBC Swahili

Croatia yatoa kitabu cha hadithi cha watoto,kinachoonyesha wazazi wenye jinsia moja

Chanzo: BBC Swahili. 


Kwa mara ya kwanza Croatia, kitabu cha watoto cha hadithi za kusimulia kitandani Kimejumuisha wahusika ambao ni wapenzi wa jinsia moja. kinajumuisha msichana aliye na baba wawili, na mvulana aliye na mama wawili. Je, unadhani kitabu kama hicho kinafaa watoto? #GNBSwahili

GNBSwahili

Kategori

Kategori