UKWELI KUHUSU ESCROW ACCOUNT WAWEKWA HADHARANI

UKWELI KUHUSU ESCROW ACCOUNT WAWEKWA HADHARANI

Taarifa zaidi kuhusu akaunti ya Escrow

TAARIFA zaidi zimezidi kupatikana kuhusu sakata la Escrow, linalohusisha makubaliano baina ya serikali, Kampuni ya kufua umeme ya Independet Power Tanzania Limited (IPTL) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama wakala wa Escrow kuwa yalikuwa ni makubaliano ya kisheria.

Makubaliano hayo yalilenga kumaliza mgogoro wa kimaslahi baina ya wabia, ambao ni Kampuni ya VIP na Mechmar kutoka nchini Malaysia, ambapo VIP ilikuwa inamlalamikia mbia mwenzake kuhusu thamani ya hisa zake.

Hali hiyo ilisababishwa na mkataba wao, ambao ulikuwa ikimtaka kampuni ya VIP kufanya kazi za utekelezaji ikiwemo misamaha ya kodi, ofisi itakayofungwa mtambo huo wa uzalishaji umeme megawati 100, ambapo mtambo huo ulifungwa Tegeta.

Taarifa zaidi kuhusu mkataba huo, ilieleza kazi zitazofanywa na Kampuni ya VIP ni asilimia 30 ya
hisa zote huku Mechmar ikibaki na hisa ya asilimia 70 kutokana na kutoa mtaji wa uzalishaji umeme.

Kutokana na hali hiyo, VIP haikuwa tayari kuanzisha mgogoro wa kimaslahi baina yake na Mechmar, wakati kesi yao ikiendelea Mahakama Kuu ndipo VIP ikatoa pendekezo la kuzuia kulipwa kwa IPTL hadi mgogoro wao utakapoisha.

Pendekezo liliungwa mkono na serikali, ambaye ni mnunuzi wa umeme kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), na kutengeneza makubaliano kisheria ya pamoja yaliyoitwa ‘Escrow Agreement’ yaliyosainiwa na pande zote tatu ikiwemo serikali, IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa kama wakala wa Escrow Julai 5, 2006.

Ilisema makubaliano hayo ya kisheria ilipelekea kufunguliwa kwa akaunti maalumu ya pamoja baina ya serikali, IPTL na BoT ili kutunza fedha zote za malipo ambazo IPTL walipaswa kulipwa kutokana na mauzo ya umeme waliokuwa wakiyafanya Tanesco kipindi chote cha mgogoro.

Katika makubaliano hayo, serikali iliingia kama mnunuzi wa umeme kupitia Tanesco na ilikuwa na wajibu wa kupeleka fedha katika akaunti ya Escrow badala ya kuwalipa IPTL moja kwa moja kama ilivyokuwa awali.

Ilieleza zaidi BoT wao walikuwa wakala wa Escrow na kazi yao ni kupokea, kutunza fedha na kutoa taarifa kwa pande zote zilizosaini makubaliano hayo huku IPTL yenyewe ikiwa ndio wazalishaji wa umeme.

Makubaliano hayo yalieleza kwamba, pindi mgogoro utakapoisha BoT itapaswa kutoa fedha hizo kwa IPTL ndani siku 60, baada ya pande zote kuafikiana.

Akizungumzia kuhusu Escrow, Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema wapo mbioni kuweka kila kitu katika wazi ili Watanzania wapate ukweli kuhusu Escrow.

Alisema Escrow lilikuwa jambo la kisheria baina ya wabia na serikali kama mpokea huduma, ambalo walilimaliza wao wenyewe kwa makubaliano yao ya kisheria.

“Hakuna kitu chochote ovu hapa, mengi yanayozungumzwa katika mitandao ni ya zamani na si mapya, ambayo yamemalizika kisheria,’’ alisema.

Hivyo, alisema IPTL/PAP ni kampuni makini isiyokuwa na chembe ya kifisadi na imefika hapo baada ya kupita hatua zote za kisheria, ikiwemo kununua hisa za VIP na Mechmar.

Alisema wanazidi kuwaomba watanzania, wawaamini na kuendelea kuwaamini kwa kuwa hakuna vitendo vya ufisadi.

source Habari Leo
MWANACHUO UDOM JELA MIAKA SITA

MWANACHUO UDOM JELA MIAKA SITA

Dar es Salaam.  Mahakama ya Wilaya ya  Ilala imemhukumu kifungo cha miaka sita jela, Melkiad Kabunduguru(28) baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kukutwa na noti bandia.
Kabunduguru ambaye ni  mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom) atatumikia kifungo hicho baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa dhidi yake.
Katika shtaka la kwanza la Kabunduguru atatumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huku shtaka la pili la kukutwa na noti 50 za bandia za Sh5000 mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Juma Hassani alisema mshtakiwa atatumikia  vifungo hivyo kwa pamoja baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Juma Hassani alidai kuwa mshtakiwa huyo atatumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za wizi.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha mashtaka, Felista Mosha uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za udanganyifu. 
“Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama hii tukufu kutoa adhabu kali dhidi ya mtuhumiwa huyu kutokana na kushamiri kwa vitendo vya udanganyifu na kujihusisha na matumizi ya noti bandia wakati akijua kuwa ni kosa la  kisheria,” alidai Mosha .
Baada ya Hakimu Hassani kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, alimuhukumu  Mwiganyi kifungo cha miaka sita jela.
Awali, Wakili wa Serikali, Felista Mosha alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 29, mwaka huu katika Barabara la Ally Hassan Mwinyi katika mashine ya kutolea fedha (ATM) ya NMB iliyopo Chuo cha Biashara (CBE) na kujipatia Sh100,000 kutoka kwa Expedith Mtisi kwa madai kuwa angemrejeshea lakini hakufanya hivyo.
Katika shtaka la pili, mshtakiwa alikutwa na noti bandia 50 za Sh5000.

SOURCE KWA HISANI YA MWANANCHI JUMAMOSI

CHADEMA YAWAACHA POLISI KWENYE MATAA



Dar/Mikoani. Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), ‘kimewaacha polisi kwenye mataa’ katika maeneo mbalimbali nchini baada ya kutojitokeza kwenye maandamano na kuwaacha askari wakiwa wamejipanga barabarani na maeneo nyeti wakiwasubiri, lakini mjini Bukoba chama hicho kilifanya maandamano.
Mjini Bukoba polisi waliojihami jana walionekana wakizunguka mitaa mbalimbali tayari kupambana na wafuasi wa Chadema, ambao waliwapiga chenga na kuandamana katika Kata ya Kibeta kwa umbali wa takribani kilometa mbili wakiwa na mabango (pichani kulia) bila polisi kuwabaini.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Gilles Muroto alisema walikuwa wamejiandaa kupambana na wafuasi wa Chadema kwa kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku nchi nzima.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Wilaya ya Bukoba, Baraka Vedasto alisema wangeandamana kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba.
Jijini Dar es Salaam, wafuasi 12 wa Chadema walikamatwa katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya chama hicho kutaka kufanya maandamano kwa makundi kufika katika ofisi hiyo.
Ulinzi ulikuwa mkali katika eneo hilo na maeneo mengine ya jiji hilo ili kuhakikisha wanakabiliana na wafuasi hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mary Nzuki alisema wanawashikilia watu hao waliowakamata eneo la ofisi za mkuu wa mkoa wakiwa na mabango. Kati yao, watano ni wanawake na saba wanaume.
“Tunaendelea kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani na tunawaomba wananchi kutii sheria bila shuruti kwani wanachokifanya ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa amani,” alisema.
Mbali na eneo hilo, askari kanzu na waliovalia sare wakitumia magari na pikipiki waliimarisha ulinzi maeneo mbalimbali hasa makutano ya Barabara ya Morogoro na Kawawa pamoja na makao makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni. Katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, askari walikuwa wamesimama katika lango la kuingilia ndani huku wakifanya upekuzi kwa watu waliokuwa wakitaka kuingia.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, “Tupo kazini kwani mpira ni dakika 90,” akimaanisha watahakikisha ulinzi unaimarishwa wakati wote.
Mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi, Ahmed Msangi alisema wafuasi na viongozi Chadema watakaothubutu kuandamana atawafanyia kitu kibaya ambacho hawatakisahau maishani.

Alisema maandamano hayo ni batili na yalipigwa marufuku kwa sababu hayana maana hivyo atakayethubutu kuandamana atakutana na kitu ambacho atakijutia.

“Nasema hivi, watu wenye akili timamu za kuchanganua mambo, wamepeleka kesi mahakamani kupinga mchakato wa Katiba, sasa Chadema kwa nini waingie barabarani kama si kutaka kuleta fujo?
“Chadema wanatuchokoza na ninasema wakithubutu kuandamana … bora nifukuzwe kazi, lakini kitu nitakachowafanyia hawatanisahau maishani mwao.”
Kwa Mkoa wa Mwanza, Chadema kimeitisha maandamano leo licha ya kutopewa kibali walichoomba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba alisema walipeleka barua polisi lakini zilikataliwa kupokewa hivyo watawahamasisha wananchi kuingia barabarani kuandamana.
Mkoani Singida, maandamano yaliyopangwa kufanyika jana yaligonga mwamba baada ya polisi kutanda katika kila barabara ambazo zingetumika.

Imeandikwa na Ibrahim Yamola, Kelvin Matandiko(Dar), Phinias Bashaya (Bukoba), Godfrey Kahango (Mbeya), Jesse Mikofu (Mwanza) na Gasper Andrew (Singida

source mwananchi jumamosi

IPTL YAMKABA KOO KAFULILA




Dar es Salaam. Sakata la tuhuma za wizi wa pesa katika Akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT) sasa limehamia mahakamani baada ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kumfungulia mashtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila.
Kafulila amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (mlalamikaji wa pili) na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth (mlalamikaji wa tatu).
Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh310 bilioni kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia pesa kutoka Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.
Kwa nyakati tofauti ndani na nje ya Bunge, Kafulila amekuwa akiituhumu PAP na Seth kuchota Sh200 biloni kutoka akaunti hiyo kupitia IPTL isivyo halali, huku pia akiwataja mawaziri na maofisa wengine wa serikalini kuhusika katika wizi huo.
Maombi ya walalamikaji
Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, walalamikaji wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe Sh210 bilioni kama fidia kutokana na kashfa hizo na hasara ya taswira ya biashara na hadhi yao.
Pia wanaiomba mahakama imwamuru mdaiwa awalipe Sh100 bilioni kama fidia ya madhara ya jumla kutokana na usumbufu walioupata kutokana na taarifa za kashfa zilizotolewa na mdaiwa dhidi yao.
Mbali na malipo hayo ya fidia, pia walalamikaji hao wanaiomba mahakama imwamuru mdaiwa awaombe radhi kutokana na taarifa hizo.
Maombi mengine ni gharama za kesi, riba kwa kiasi cha pesa yote wanayodai kwa kiwango cha asilimia cha mahakama, kutoka tarehe ya hukumu hadi tarehe ya mwisho wa malipo hayo na amri nyingine ambazo mahakama itaona zinafaa.
Inaeleza kuwa kutokana na mgogoro huo, kiasi cha Sh200 bilioni ziliwekwa katika Akaunti ya Escrow iliyofunguliwa BoT, kusubiri kumalizika kwa mgogoro wao huo uliokuwa mahakamani hapo.
Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa mgogoro huo ulimalizika na kuhitimishwa kwa mdai wa kwanza (IPTL) kupata amri ya mahakama kumiliki pesa hizo na BoT kutakiwa kuziachia.
Hati hiyo inaeleza kuwa katika hali ya kushangaza na pasipo na uhalali wowote, madaiwa katika matukio tofautofauti na nje ya Bunge aliamua kusambaza kwenye mitandao ya kijamii taarifa za kashfa dhidi ya mdai wa kwanza na mdai wa tatu.
Mitandao hiyo ya kijamii iliyotumika kusambaza kashfa hizo kwa mujibu wa hati ya madai, ni Jamii Forum, Twitter Facebook.
Hati hiyo ya madai inaeleza kuwa Juni, 2014, mdaiwa alichapisha kuwa mdai wa kwanza na wa tatu walijipatia pesa kutoka akaunti ya Escrow isivyo halali, wakati si kweli.
“Mdaiwa bila uhalali wowote alisambaza taarifa kuwa, mdai wa kwanza amehusika katika vitendo viovu vya kuchukua pesa hizo katika akaunti ya Escrow, jambo ambalo halina ukweli,” ilisomeka hati hiyo.
Pia inadai kuwa mdaiwa amekuwa akitoa taarifa za kashfa huku akimtaja mdai wa tatu kuwa ni Singasinga, jambo ambalo si sawa na hivyo kuharibu sifa yake na kusababisha uendeshaji wa biashara zake zinazotekelezwa na mdai wa kwanza na wa pili kudorora.
Hati hiyo ya madai inaeleza kuwa kitendo cha mdaiwa kutoa taarifa hizo za kashfa kimesabisha jamii kwa jumla kuamini kuwa kweli mdai wa kwanza amejipatia pesa hizo kutoka katika akaunti hiyo isivyo halali na kwamba raslimali zao zinahujumiwa na mdai wa kwanza.
“Zaidi kitendo cha mdaiwa kutangaza kwa jamii taarifa za mdai wa kwanza kujihusisha na mchezo mchafu kimesabisha hasara au kupungua kwa hadhi ya mdai wa kwanza na wa pili.”, inabainisha hati hiyo ya madai.
Inaendelea kueleza kuwa mdaiwa akiwa ni mbunge ana kinga ya kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa yale aliyoayasema bungeni, lakini pia inabainisha kuwa taarifa hizo za kashfa zimesambazwa na mdaiwa nje ya bunge.
Hati hiyo ya madai inaisisitiza kuwa kitendo cha mdaiwa kuchapisha na kusambaza taarifa hizo kwa jamii si tu kwamba kimeshusha hadi ya mdai bali pia kimesabisha hasara ya kibiashara.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, mdaiwa bado anaendelea kutangaza taarifa hizo za kashfa dhidi ya wadai, licha ya taarifa ya maneno nay a maandishi aliyopewa, hivyo kusabaisha hadhi ya wadai kuendelea kushuka na kusabisha hasara ya kibiashara.
Inadai katika hati hiyo kuwa hadhi yao si tu kwamba imeshuka nchini bali pia kimataifa na hivyo kuwasabishia hasara kibiashara, na kwamba taarifa hizo pia zimewasababishia madhara ya kisaikolojia na usumbufu kwa menejimenti nzima.
Inaeleza kuwa kitendo cha mdaiwa kuelezea mambo yaliyojiri katika mahakama za kisheria katika maombi baina ya mdai wa kwanza na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited kimesabaisha si tu kuingilia uhuru wa mahakama bali pia hasara kwa mdai wa kwanza.
Wadai wanaendelea kueleza kuwa mdaiwa alikuwa akijua kilichoendelea mahakani katika maombi hayo baina ya mdaiwa wa kwanza na VIP, lakini aliamua kutangaza kinyume kuhusu akaunti ya Escrow.
Hati hiyo inasisitiza kuwa mdai wa kwanza alipata pesa hizo kutokana na amri halali ya mahakama baada ya uamuzi wa maombi hayo baina yake (IPTL) na VIP.
Inaendelea hati hiyo kudai kuwa kwa kuwa mdaiwa wa kwanza anatoa huduma ya kulisambia Tanesco umeme, taarifa hizo za mdaiwa zimejhatarisha uhusiano baina yake (mdai) na Tanesco na hivyo kusabaisha kudorora kwa uchumi na biasha ya wadai.
Alichokisema Kafulila Bungeni
Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2014/15, Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kamapuni ya Pan African Power Solutions (PAP).
Alisema kuwa kampuni hiyo ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu kwa ya “Singasinga na kwamba ni ya kitapeli.
Alifafanua kuwa kampuni hiyo iliidhinishiwa pesa hizo kwa udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo sio la kweli.
Mbali na Kampuni hiyo aliwahusisha Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Waziri wa Fedha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na vigogo wengine wa BoT na wa serikalini.
Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki kuu mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia dola milioni 122 za Marekani,” alisema Kafulila.
Alisema kuwa fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.
Alifafanua kuwa IPTL ilikuwa ni makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ya Malaysia ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.
Kafulila alisema kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP tu na kwamba hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

MAKALA:Wasira anatumia kigezo gani kuutamka ushetani wa wapinzani


Wakati joto la uchaguzi 2015 likiendelea  kupanda nchini, propaganda za kuwachafua wapinzani zinazidi kuongezeka.
Viongozi  wa Serikali ya CCM  wanaendelea kukitetea chama chao kwa kila njia.
Mbinu inayoonekana kutumiwa  chama hicho tawala ili kushinda uchaguzi ni propaganda katika  vyombo vya habari na matumizi mabaya  ya dini.
Gazeti la moja wiki iliyopita liliandika habari yenye maneno ya kufuru likimnukuu mwanasiasa mkongwe  nchini, Stephen Wasira wakati akimsimika kamanda wa vijana  Kata ya Butimba.
Wasira alinukuliwa akisema kwamba upinzani mamlaka yao ni ya kishetani na kwamba CCM mamlaka yao ni ya kutoka kwa Mungu aliye mbinguni.”
Najiuliza je, Wasira anamfahamu shetani au anamsikia?  Je, Wasira anamjua Mungu kweli na sifa za Mungu anazijua hadi atamke hivyo? Je, anazijua mamlaka hizi mbili vizuri?
Hii inaonyesha wazi  kwamba  CCM wanayo ile dhana  kuwa “Kikwete ni chaguao la Mungu” na hivi chama chao ni chaguo la Mungu pia.
Niliposoma  habari hiyo nilitafakari sana na nikahitimisha kwa kusema kwamba baadhi ya watu ndani ya CCM wanaendelea na mchezo wao wa kumkufuru Mungu aliye juu mbinguni kwa mithili ya mnara wa Babel.
Nikiwa natafakari kauli ile ya Wasira, nikakumbuka mahubiri ya padre mmoja alikuwa anahubiri juu ya shetani kanisani  na akawauliza waumini wake: “Je, nani anamjua shetani,  nani   amewahi kumwona na kama  umewahi kumwona  tuambie anafananaje?”
Baada ya dakika kama tatu  kupita  kanisa lote lilikuwa kimya kabisa kama vile ni malaika anapita. Wale waliokaa mbele  walikuwa wanainama  wasije wakagongana macho na padre na kuwaambia waeleze.
Padre aliamua kurudia  swali lake, lakini hakuna aliyejitokeza kujaribu kumjibu. Kwa nini waumini wote waliogopa kumjibu padre swali hili?
Padre aliamua kutoa jibu mwenyewe na akasema “Shetani pia ni mimi na wewe, kwa matendo yetu maovu.” Padre hakumwonyesha  muumini yeyote kama ni shetani hata kama anajua kuna watu wanatabia za kishetani.
Ni kwa mantiki hii, najaribu kujiuliza hivi Wasira anamjua shetani au anamsikia tu? Anatumia kigezo gani kuutamka ushetani wa wapinzani?
Vitabu vitakatifu vinatufundisha kuondoa kwanza boriti katika macho yetu ndipo tuweze kuona kibanzi kwa mwingine. Siasa si matusi, kejeli, utekaji, wala ugomvi, vita na mauaji la hasha!
Lakini huko tunakoelekea  hasa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kuna kila  dalili  za nchi ya Tanzania kukosekana kwa utulivu endapo siasa za kibabe zitaendelea kushabikiwa.
Kuwaita wapinzani  mashetani ni kuonyesha upeo  mdogo  wa kujenga hoja na hivyo kutaka kutumia mafundisho ya dini  kufanya siasa chafu.
Haya ni matumizi mabaya ya elimu ya imani na huku ni kuvuka mipaka iliyopitiliza. 
Kama CCM ina  mamlaka kutoka juu kwa Mungu,  kwa nini Tanzania kuna matatizo mengi sasa.
Kwa nini albino wanauawa kila siku, mabilioni ya fedha yanaibwa na watu wanaofahamika lakini mamlaka ipo tu, ajali za barabarani ndiyo hizo, mauaji ya kisiasa  yamejaa nchini, uvunjaji wa haki za binadamu ni kitu cha kawaida, wizi wa tembo na wanyamapori, mauaji ya raia wasio na hatia, uchomaji wa nyumba za ibada na uchakachuaji wa mchakato wa Katiba, je, hayo ndiyo mamlaka ya kutoka kwa Mungu?
Ni wazi Wasira  anajaribu kufanya propaganda (porojo za kisiasa) kuwadanganya  Watanzania wasiojua neno la Mungu na maana halisi ya shetani.
Kati ya wapinzani na CCM ni chama gani kina mambo yanayokwenda kinyume na matarajio ya wengi? Kuvuruga maoni na mawazo ya wananchi  wa Tanzania na kubandika mawazo yao katika Katiba Mpya je, hilo si jambo la kishetani?
Kwa sababu kuna usemi usemao sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Wasira haoni hapa anapingana na mamlaka ya Mungu ambaye ni Mungu wa watu wote na hasa  wale maskini, wanyonge  wasiokuwa na sauti?
Ndiyo maana nauliza hivi, Wasira anamjua shetani au anamsikia?
Watanzania wa leo hawawezi kuendelea kudanganywa tena na wanasiasa, huu ni muda wa mabadaliko ambayo hakuna nguvu itakayoweza kuzuia mabadiliko hayo.
Kuonyesha hali ya kutoijua demokrasia na utawala bora Wasira alinukuliwa  akisema CCM  itahakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kutawala Tanzania.
Mungu halazimishi mipango yake kamwe na wala Mungu halewi madaraka na kutumia ubabe  na vitisho kama inavyofanya na baadhi ya wanasiasa. Bali, shetani huwa anatumia mbinu chafu, hila, fitina, mauaji, uongo, vitisho, jeuri ili kumtawala mwanadamu.
Baadhi ya watawala hawajali maisha ya wananchi. Wanachojali ni wao kuendelea kuwatawala wananchi maskini na wanyonge na waoga wakisifiwa kwa kigezo cha kuwa ni watiifu na wapenda amani.
Kumbukeni mtu mwenye mamlaka ya Mungu ana heshimu wanadamu, lakini baadhi ya watawala hawana heshima kwa Watanzania. Ushahidi ni jinsi ilivyochakachua maoni ya wananchi ya Rasimu ya Warioba.
Mamlaka ya kutunga Katiba Mpya kama ni sehemu ya Mamlaka ya Mungu kama anavyojigamba Wasira, basi  Mungu huyo ni wa kuchongwa na siyo Mungu kama tunavyomjua yaani mpole, mwenye  huruma, mtenda haki, mpenda maskini na kadhalika.
 Baadhi ya watawala waache kutumia maneno ya Mungu kuhalalisha   ulevi wa madaraka kwa sababu Mungu atakapogeuza kibao hamtasalimika.
Mungu hapendi utawala wa mabavu  na vitisho kama wanavyofanya baadhi yao.
SOURCE Mwananchi

KATIBA MPYA:Bunge kutuma ofisa Saudia kusimamia kura





Dodoma. Ofisi ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo wanaokwenda Hijja.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.
Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya Uongozi jana.
Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.
Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado haijajulikana.
Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu.
Alisema ni vigumu kutaja vituo watakavyopigia kura sasa kwa sababu bado hawajawauliza wajumbe wengine waliopo nje ya nchi ambao wangependa kupiga kura wakiwa huko.
Kuhusu iwapo watapiga moja kwa moja kwa mtandao au watapiga kwenye karatasi na kutoa vivuli, Hamad alisema suala hilo litaamuliwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge chini ya Mwenyekiti, Samuel Sitta.
Ukawa wapinga
Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba na James Mbatia wamelishukia Bunge hilo kwa kuruhusu upigaji kura nje ya nchi.
Akizungumza jana, Profesa Lipumba alisema kilichofanywa na Sitta na wajumbe wake ni uchakachuaji unaoweza kuliingiza Taifa kwenye mgogoro mkubwa.
“Kwanza taratibu za kura mabunge ya Jumuiya ya Madola ni kura zote zinapigwa ndani ya Bunge. Unapozungumzia akidi imetimia ni wajumbe walioko ndani ya Bunge,” alisema Profesa Lipumba.
Kanuni mpya ya 30 (1) baada ya marekebisho yaliyofanyika juzi inasomeka, “Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalumu itakuwa ni nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu.”
Awali, kanuni hiyo iliweka sharti la lazima kwamba akidi ya kikao itakuwa ni nusu ya wajumbe, isipokuwa kwa kikao kinachohusu kupitisha uamuzi wa Bunge Maalumu.
“Mwenyekiti hawezi tu kutangaza kuwa akidi imetimia kwa sababu nimepata barua kuna wajumbe wako nje kwa hiyo watapigia kura huko. Ni uvunjifu wa sheria na taratibu ulio wazi,” alisisitiza.
“Hakuna maridhiano lakini zaidi ya hapo huu mchakato wote umeshaharibika. Kinachofanyika hapo ni Sitta kujaribu kuhalalisha matumizi ya Sh20 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo,” alisema.
Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema kinachofanywa na Sitta ni kuhakikisha wanatoka na Katiba hata kama haina uhalali wa kisiasa.
“Kwa hiyo inabidi lazima atoke na kitu ili aseme tumepitisha uamuzi tumetoka na Katiba hii ili kuhalalisha matumizi,” alisema Lipumba na kuhoji uharaka huo wa Sitta ni wa nini?
“Kama muda hautoshi kwenda kwenye kura ya maoni kulikuwa na sababu gani ya kuendelea na mchakato huo. Mchakato wa Katiba unakwenda katika utaratibu wa sheria,” alisema.
Profesa Lipumba alisema sheria iko wazi na iliweka utaratibu kuwa baada ya kupatikana kwa Katiba inayopendekezwa, isipite siku zaidi ya 120 bila kura ya maoni kufanyika.
“Ni wazi sheria yenyewe itabidi ibadilishwe. Rais atakayekuja akiwa makini hawezi kukubali kuanza na Katiba iliyowagawa Watanzania. Rais gani atakubali kuanza na migogoro ya kisiasa?” alihoji Lipumba.
“Waziri wa Katiba wa SMZ (Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) hashiriki, AG (Mwanasheria Mkuu) wa Zanzibar hashiriki Katiba ya nchi, watu wa Zanzibar hawashiriki utasemaje ina uhalali wa kisiasa?”
Mbatia alisema anamshangaa Sitta kujigamba kutoka na Katiba inayopendekezwa wakati itakwenda kukaa kabatini kusubiri utashi wa rais ajaye.
“Hatuna kura ya maoni kwa hiyo haiwezi kutumika. Kwa hiyo ikishapokewa inawekwa kabatini. Rais ajaye ni mwingine, sisi tunaendelea na mikakati yetu ya marekebisho ya 15 ya Katiba,” alisema.
Kuahirishwa kwa kura ya maoni kunatokana na makubaliano kati ya viongozi wa Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD) na Rais Jakaya Kikwete yaliyofikiwa Septemba 8, mwaka huu
source:Gazeti la Mwananchi Jumanne

CAG ATAKA UHURU WA OFISI YAKE



Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovic Utouh
amewataka wafanyakazi wa ofisi hiyo kuhakikisha Katiba ya nchi inaimarisha na kutunza uhuru
utendaji wa ofisi hiyo.
Utouh ambaye anastaafu wadhifa huo baada ya kutimiza umri wa miaka 65, alisema hayo katika
 hafla ya kumuaga iliyofanyika juzi mjini Dodoma ambapo alionya kuwa bila kuwa na uhuru huo
katika utendaji, huenda mambo yasiende kama inavyotarajiwa.

“Hakikisheni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaimarisha na kutunza uhuru wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,” alisema CAG Utouh huku akiwataka wakaguzi wajipange kwa kusoma zaidi na kuwa wabunifu hasa kipindi hiki ambapo nyanja hiyo inapanuka na kubadilika kwa kasi hasa kipindi hiki ambacho gesi imegundulika huku utafiti
kuhusu mafuta ukiendelea

“Nyanja ya ukaguzi inabadilika, kuna ukaguzi unaotakiwa ufanywe katika miradi ya gesi, mafuta, mazingira, menejimenti na fani nyingine ambazo ni mpya,” alisema na kuongeza: “Yote hayo msingi wake ni kusoma kwa bidii na siyo kubweteka.”

Akizungumzia historia ya ofisi hiyo, Utouh alisema kuwa alipoingia kwenye ofisi hiyo aliikuta inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo uhaba wa wafanyakazi na kwamba katika miaka minane wameongezeka kutoka 493 hadia 814, ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 65.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alimsifu CAG kwa kuimarisha miundombinu ya kiutendai hali ambayo iliongeza idadi ya wahasibu na kuifanya Serikali kutafuta miundo na mifumo katika ngazi ya kimataifa.

“Hongera…, umesaidia kuongezeka kwa weledi wa kiuongozi na kiutendaji serikalini, mifumo ya kiutendaji, uwazi na upatikanaji kwa urahisi wa taarifa za msingi kwa jamii sanjari na ushirikishwaji wa wananchi ambao sasa ni mkubwa tofauti na awali,” alisema Makinda

SOURCE GAZETI LA MWANANCHI
MAANDAMANO YA UKAWA YAPINGWA

MAANDAMANO YA UKAWA YAPINGWA

Na Khamis Amani
Katiba bora yenye maslahi kwa pande zote mbili za Muungano haitaweza kupatikana kwa maandamano yenye kuashiria uvunjifu wa amani.

Diwani wa wadi ya Kwahani wilaya ya mjini Unguja, Machano Mwadini Omar, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya mchakato wa katiba mpya unaoendelea.

Alisema wananchi wanapaswa kufahamu lengo la mchakato wa katiba unaoendelea ni kupatikana katiba itakayosimamia mwenendo wa serikali zote mbili zilizounda Muungano.

Alisema upatikanaji wa katiba hiyo utaondosha malalamiko kutokana na kila upande kupata fursa sawa zitakazosimamia kuendesha serikali zao na wananchi wake kwa ujumla kwa misingi ya haki na usawa.


Alisema, katiba hiyo haiwezi kupatikana nje ya vikao vya Bunge Maalumu kwa kuitisha maandamano.

Alisema, kitendo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia vikao vya Bunge maalumu na kuitisha maandano sio cha busara, kwani hali hiyo haiwezi kusaidia kupata katiba.


Alisema, wajumbe wa Bunge Maalumu ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo na makundi yao, hivyo ni vyema kutumia fursa hiyo kuwaitikia na kuwawakilisha ipasavyo wananchi hao ili waweze kupata katiba itakayosimamia haki zao kwa mujibu wa sheria.

PINDA: KUTAJWA URAIS NI VYEMA


Dodoma. Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa siyo jambo baya kwake kutajwa kutaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015 na kwamba kujitokeza pia ni jambo jema.
 Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, ambapo alizungumzia mambo mbalimbali, Pinda alisema kuwa jambo la msingi kwa wote wenye nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini ni kutambua kuwa urais ni dhamana kutoka kwa wananchi na haupatikani kwa uamuzi wa anayegombea, bali taratibu za vyama na wananchi watakaopiga kura.
 Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima alisema pia kwamba ni muhimu kwa watu wanaotaka kuwania urais wasikiuke misingi ya haki kwa kuingilia mchakato na kuwadhoofisha watu wenye mamlaka ya kuchagua mgombea urais, bali waachwe ili wafanye uamuzi wa haki kwa manufaa ya taifa, huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Kujitokeza ni jambo jema, kutajwatajwa nako pia ni jambo jema tu kwa maoni yangu. Ninachoweza kusema kikubwa, wote wanaotaka kwenda kwenye hiyo nafasi, rai yangu kubwa ni moja tu, watambue wanachotaka kwenda kufanya ni dhamana. Ni nafasi kubwa, lakini ni dhamana tu unapewa kwa niaba ya Watanzania wengine wote.
“Kwa hiyo basi, uamuzi wa nani atakuwa, hauwezi kuwa wa kwako wewe. Lazima tuuache mikononi mwa wale ambao kikatiba, kisheria na kadhalika, ndiyo wamepewa hilo jukumu. La msingi hapa sisi ambao tunataka kuingia kwenye dimba hilo, tuhakikishe hatuwadhoofishi katika kufanya uamuzi wao wa haki kwa vishawishi, kwa vivutio, tuache wafanye uamuzi kwa imani kwamba wanayemchagua atatufikisha pale ambapo tunataka,” alisema Pinda.
Alifafanua: “Mimi sisomi sana mtandao, lakini wakati mwingine nalazimika kusoma, kwa msingi huo hakuna haja ya kurushiana maneno au kuchukiana kwa wanaotaka kugombea, kwani kati yao, hakuna mwenye uhakika wa nani atakuwa. Kila mmoja anasema nami nijaribu, unakwenda huko na moyo mweupe, kimtazamo ambapo unafanya kazi kihalali, kwa haki, kiuadilifu, lakini mwishowe tujue kwamba uamuzi unabaki kwa watu waliopewa dhamana ya kuteua mgombea katika hatua ya mwisho. Tukiwapa fursa hiyo, naamini tutapata kiongozi mzuri.”
Hivi karibuni vyombo vya habari viliandika habari zilizodai kuwa Waziri Mkuu Pinda alitangaza nia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015, akiwa mkoani Mwanza. Wengine waliotangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM ni January Makamba, ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, na Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla.
Wengine wanaotajwa katika mbio hizo ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa,  Samuel Sitta (Spika wa Bunge Maalumu la Katiba), Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose- Migiro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira, Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Wingi wa wagombea
Akizungumzia wingi wa wanaojitokeza kutaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa taifa kupitia CCM, Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa siyo jambo baya akisisitiza kwamba jambo muhimu ni kuachia wenye dhamana ya kuchagua mgombea, lakini akasema tatizo linaweza kutokea iwapo makundi hayo yatagombana.
Alisema kwamba katika CCM siyo jambo gumu kurudisha pamoja makundi tofauti ya waliowania nafasi ya kuteuliwa baada ya mmojawao kuteuliwa na chama kukiwakilisha katika uchaguzi mkuu, huku akisisitiza kuwa kama makundi yatagombana na kutukanana ndipo ugumu hutokea.
“Changamoto zitakazojitokeza pengine kwenye chama ni namna ya kurejesha wale wote ambao walikuwa wana mtu wao waliyekuwa wakimfanyia kampeni. Hakuna tatizo kurudisha kundi, tatizo linaibuka tu kama kundi moja limekuwa linagombana na lingine,” alisema na kufafanua:
“Kwa hiyo mnabaki kazi yenu kushambuliana, akija kupata mmoja, mwenzake anapata kigugumizi anasema; huyu si alikuwa akinishambulia, sasa nitawarudishaje kundini?
“Lakini kama wote tutakwenda na dhamira moja ni rahisi kusema, bwana mimi nilikuwa huku na sikufanikiwa, naomba tumuunge mkono bwana huyu ambaye amepewa dhamana na wenye mamlaka ambao ni wananchi, hapo ni rahisi. Tukifanya hili ‘braza’ hakuna mgogoro hata kidogo,” alisema Pinda.

Nguvu yake ipo kwa Mungu
Alisema kwamba katika yote anayofanya siku hadi siku hana tumaini lingine zaidi ya kuwezeshwa na Mungu, akibainisha kuwa husali kila anapolala na kuamka salama, akikabidhi majukumu yake mbele ya Mungu ili amwezeshe kufanikiwa.
“Ni kweli mambo ni mengi, lakini kikubwa ambacho nasema, siku zote napata faraja  katika kuamini nguvu za Mwenyezi Mungu. Mimi ndiyo imani yangu. Kila ukiamka salama unasema; ee Mwenyezi Mungu nashukuru leo umeniamsha salama, naomba leo unijalie niwezeshe kutekeleza majukumu yangu, hata kama nikitetereka lakini narudi kwa Mungu,” alisema Pinda. Alitaja jambo la pili ambalo pia nguvu yake ni namna anavyoshirikiana na wenzake katika utendaji kazi wa siku kwa siku akiwa karibu na watendaji na wasaidizi wake aliowasifu kuwa wanamsaidia kwa kiasi kikubwa hata kubaini mambo na matatizo yanayojitokeza ambayo pengine yeye binafsi asingeweza kuyabaini. Pia ukaribu na watu mbalimbali na jamii ni mambo ambayo husaidia kujenga uwezo.
“La tatu, kwa sababu nimekulia serikalini, Ikulu, hata nilipopata ubunge nilipewa unaibu waziri wa Tamisemi pale Ikulu, baadaye waziri sasa Waziri Mkuu. Hili llimenipa uzoefu, kuijua Serikali na kuwa karibu na chama, kuniwezesha kukijua chama pia kuijua nchi kwa jumla na kuwa mwepesi kupokea ushauri. Kuwa tayari kupata ushauri kwangu siyo dhambi,” alisema Pinda akihitimisha:
“Nadhani ukichanganya yote hayo na baraka zenu nyie mnaotutakia mema, nadhani mambo yatakwenda vizuri.”
SOURCE:MWANANCHI JUMAPILI

CHADEMA kumekucha,MGOMBEA UENYEKITI AJITOA





Hamkani hali si shwari ndani ya Chadema! Kansa Mohamed Mbaruku, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Tabora, amejitoa kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa, hivyo kumfanya kwa mara nyingine Freeman Mbowe kuwa katika mashindano ya 'farasi' mmoja.

Kwa mujibu wa 'Mwananchi Breaking News', Mbaruku ameamua kujitoa kwa madai kwamba katiba ya chama hicho imekiukwa na akasema atakwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga uchaguzi huo na kuomba ufafanuzi wa kikomo cha uongozi.
Mbaruku amejitoa siku moja tu baada kabla ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake, ambao umepangwa kufanyika kesho Jumapili Septemba 14.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba kujitoa kwa mgombea huyo kunaweza kusababisha mpasuko ndani ya Chadema kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya uongozi kwamba unaendesha chama kama 'taasisi binafsi'.
Awali Mbaruku aliwasilisha pingamizi kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, ambapo pamoja na mambo mengine, alidai kwamba Mbowe hana sifa kikatiba ya kugombea tena nafasi
hiyo.

Pia duru za siasa ndani ya chama hicho zilieleza kwamba, majina mawili yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda katika chama hicho, Benson Kigaila, kwamba nao walijitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti, Daniel Ruvanga na Garambenela Frank, yalikuwa majina hewa yaliyolenga kumsafishia njia Mbowe ya kubakia kuwa mgombea pekee baada ya kuenguliwa kwa Mbarouk.
Inaelezwa kwamba, Katiba ya Chadema hairuhusu kiongozi wa nafasi hiyo kugombea vipindi zaidi ya viwili vya miaka mitano.

source:brother danny blogspot.com

KIMENUKA CCM VS CHADEMA


Mbunge wa jimbo la Mpendae CCM Salim Turki amekidharirisha, kukifedhehesha, na kukitukana Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kusema kwamba ni chama cha watu wasio na akili ,wasio na misingi na kwamba CCM inaweza kuwafanya lolote na wasifanye kitu.

Mbunge huyo amewadharirisha CHADEMA mbele ya kikao cha usuluhishi baina ya Upande wao na wenzao kilichofanyika Central polisi hivi karibuni,mbele ya Maafisa waandamizi wa polisi,ambapo aliitwa pamoja na upande wa pili ambao wanaopingana kujadili namna ya kutatua mgogoro wao.

Aliwafananisha anaopingana nao sawa na CCM wanavyowanyanyasa CHADEMA bungeni na kwamba sauti yao haina pa kusikika na wasio na lolote wala chochote.
Hii ni dharau kubwa kufanywa na Mbunge kwa CHADEMA.

CHADEMA MPOOO!

ONA VIDEO HII
 Source:facebook

BUNGE LA KATIBA LAPUMULIA MASHINE


HATUA ya kujiondoa kwa Mwanasheria Mkuu wa  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman katika ujumbe wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, huku waziri wake, Abubakar Khamis Bakari akiwa amesusia Bunge Maalumu la Katiba kwa muda sasa, imezidi kuliweka pabaya Bunge hilo.
Pamoja na hayo, kuongezeka kwa shinikizo la kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutumia mamlaka yake kusitisha Bunge hilo kutokana na kitendo cha  Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vyake, huku wajumbe wanaondelea na vikao vyake mjini Dodoma wakibadili maudhui yaliyomo kwenye Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba, 
kunatafsiriwa kama ni hatua ya Bunge hilo kuelekea ukingoni.
Baadhi ya wanasheria waliozungumza na gazeti hili, wamesema kitendo cha viongozi hao waandamizi na muhimu katika usimamizi wa sheria na Katiba kwa upande wa SMZ kususia mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba, ni kiashiria tosha cha mwelekeo wa kukwama ama kuvunjika kwa Bunge hilo.
Mwanasheria maarufu na mjumbe wa Ukawa, Profesa Abdallah Safari, alisema kitendo hicho kinaashiria hatua mbaya ya mwelekeo wa Bunge Maalumu la Katiba.
Profesa Safari amekitafsiri kitendo hicho na jahazi linaloelekea kugonga mwamba, hivyo manahodha wameamua kujitosa baharini ili kunusuru maafa zaidi.
“Viongozi hawa ni muhimu, lakini kujiengua kwao kunanikumbusha ajali ya kuzama kwa meli ya Titanic, kwamba Bunge linakoelekea lazima litagonga mwamba na kusababisha maafa makubwa, hivyo wameona wajitose baharini kwa kuepusha maafa zaidi… Unajua AG ni mtu mkubwa sana kujiondoa katika Kamati ya Uandishi wa Katiba,” alisema Profesa Safari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo Bi-Simba, ameizungumzia hatua hiyo kuwa inatokana na Bunge hilo kukosa mwelekeo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutokea nchini India, Kijo Bi-Simba alisema kitendo cha viongozi nyeti, tena wanaosimamia sheria na Katiba kwa upande wa Zanzibar kujitenga na mchakato wa Katiba mpya, kinaibua hisia za kuwapo kwa tatizo ndani ya Bunge Maalumu la Katiba.
“Sipo nchini, lakini habari hiyo imenishtua, ni bora Bunge hili lisitishwe kwanza kwa ajili ya kutafuta maridhiano ya kisiasa, kiukweli limeingiwa na doa baada ya Ukawa kususia, kwahiyo hawawezi kulilazimisha liendelee kwani litazalisha matatizo makubwa kwa nchi,” alisema.
Wakili wa kujitegemea, Peter Kibatala, alisema sheria inapaswa kutafsiriwa kwanza na mahakama ili itelezwe katika mstari ulionyooka.
Hatma ya kuendelea ama kutoendelea kwa Bunge hilo inatarajiwa kujulikana kesho mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mwisho cha kutafuta mwafaka wa mchakato wa Bunge hilo ambacho kinawakutanisha Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Ukawa.
Tayari msimamo wa Ukawa ni kutaka Bunge hilo lisitishwe, na Katiba ya sasa ifanyiwe maboresho, hasa kwenye vipengele muhimu kama matokeo ya uchaguzi wa rais kupingwa mahakamani, kuwapo Tume Huru ya Uchaguzi na kuruhusiwa mgombea binafsi.
Kutokana na mwenendo wa hayo yote, mmoja wa viongozi wanaounda Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na MTANZANIA Jumapili alisisitiza rai yake ya kumtaka Rais Kikwete asitishe Bunge hilo kwa kile alichodai kuwa muda hautoshi wa kupatikana kwa Katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
“Siku tulipokutana na rais alikuwa msikivu, mkarimu na alitusikiliza. Jumatatu tutakutana kwa ajili ya kikao chetu cha mwisho ili kupata mwafaka kwa sababu muda wa kupatikana kwa Katiba kabla ya uchaguzi mkuu hautoshi tena… tulipeana majukumu ikiwamo kubadilishana mawazo, kuangalia sheria na taratibu kwa sababu sisi nia yetu ni njema kabisa ya kuendeleza demokrasia,” alisema Profesa Lipumba.
Kauli hiyo ya Profesa Lipumba ndiyo inaakisi kile kinachodaiwa kujiri ndani ya kikao cha Rais Kikwete na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia (TCD) wakiwamo Ukawa, ambacho kilifanyika katikati ya wiki hii.
Kwamba gazeti hili lilidokezwa kuwa rais alionyesha kukubaliana na hoja ya kufanyiwa marekebisho kwa Katiba iliyopo ili itumike katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Kauli kama hiyo imewahi kutolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, aliyesema kwamba ikiwa mchakato wa kupata Katiba mpya utakwama, Katiba iliyopo itafanyiwa marekebisho hasa katika vipengele vinavyopigiwa kelele ili itumike katika uchaguzi mkuu ujao.
Mbali na hayo, Jukwaa la Wakristo Tanzania linaloundwa na Baraza Kuu la Kanisa Katoliki (TEC), Jumuiya ya Wapentekoste (CPCT), Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT) na Wasabato (SDA) nalo hivi karibu lilitoa tamko la mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba kwa kumtaka Rais Kikwete achukue hatua za kusitisha vikao vyake.
Hoja kama hiyo pia imewahi kutolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akipendekeza Bunge hilo lisitishwe kwa sababu limekosa mwelekeo.
Hatua ya sasa ya Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman kujiweka kando na kamati hiyo inayoelezwa kuwa ni moyo wa Bunge hilo katika kuandika Katiba mpya itakayopendekezwa imeziongezea nguvu hoja hizo.
CCT YAWAKANA VIONGOZI WA DINI BUNGE LA KATIBA
Wakati huo huo, katika kile ambacho kinaweza kutafsiriwa kuwa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imelivua nguo Bunge Maalumu la Katiba, ni hatua yake ya kuwakana wajumbe wa Bunge hilo wanaodai kuteuliwa kuwakilisha taasisi za dini.
Katika tamko lake ililolitoa jana kwenye vyombo vya habari, CCT imedai kumtambua mwakilishi wao mmoja tu waliyemtaja kwa jina la Esther Msambazi, wakimwelezea kama Mkristo wa kawaida (lay Christian) wala si kiongozi wa dhehebu lolote la wanachama wa CCT ama mzee wa kanisa.
Wachungaji na maaskofu walio mdani ya Bunge hilo ni Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Donald Leo Mtetemela, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ernest Kadiva na Askofu wa Kanisa la Memonite Dayosisi ya Kati Dodoma, Amos Muhagachi.
CCT ilisema viongozi wengine wa dini ya Kikristo (maaskofu na wachungaji) waliopo katika Bunge hilo hawakuwatuma na hawana taarifa walichaguliwa kwa njia ipi kuwa wajumbe.
“Kama ambavyo ilitangazwa na rais, Januari 2014 kuwa taasisi zipeleke mapendekezo ya wajumbe wanaoweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, CCT ilipeleka wajumbe tisa ambao kati yao, mjumbe mmoja tu ambaye ni Esther Msambazi aliteuliwa.
“Viongozi wengine wa dini ya Kikristo (maaskofu na wachungaji) waliopo katika Bunge hilo hawakutumwa na CCT na wala CCT haina taarifa ni vipi walichaguliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo Maalumu,” lilieleza tamko hilo.
CCT walisema hawawatambui viongozi hao, kutokana na Jukwaa hilo kuundwa na taasisi za TEC, CCT, PCT na SDA ambao kwa pamoja huafikiana masuala yao na kamwe hawapingani.
“Kutokana na misingi ya imani ya taasisi hizi kwa umoja wake, viongozi wakishakubaliana jambo fulani kwa pamoja na kwa umoja wao wanalisimamia na kulitekeleza. Ndiyo yao ni ndiyo na hapana ni hapana kwa kuwa hawana ndimi mbili na wala hawatumikii mabwana wawili,” lilisema tamko hilo.
Taarifa hiyo ilisema CCT ikiwa mmoja wa taasisi zinazounda Jukwaa la Kikristo nchini inasisitiza kuwa msimamo wa viongozi wa dini kama ulivyotolewa na Jukwaa hilo kuhusu maoni waliyopeleka kwa tume iliyokuwa chini Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba pamoja na matamko yaliyotolewa ni sahihi na itaendelea kuyasimamia.
Pia CCT ilisisitiza haiwezi kufuata maoni ya viongozi wa dini walioko bungeni kutokana na kutowatambua na pia kukataa watakayokuwa wakiyasema.
Hivi karibuni Jukwaa la Wakristo lilitoa tamko, pamoja na mambo mengine lilipinga kuendelea kwa Bunge la Katiba kwa madai ya kuhodhiwa na chama tawala hoja ambazo zilipingwa na wawakilishi kutoka kundi la 201 waliodai kuwakilisha taasisi za dini.

Kuhusu mwandishi


MGOGORO BUNGE LA KATIBA


Dodoma. Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kukutana tena na viongozi wa vyama vya siasa ambavyo ni wanachama wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), kuna taarifa kwamba huenda Oktoba 4, mwaka huu ikawa siku ya mwisho ya kukutana kwa Bunge Maalumu, linaloendelea na utunzi wa Katiba Mpya mjini Dodoma.
Mkutano wa Rais Kikwete na viongozi hao kutoka vyama vyenye wabunge na kimoja kinachowakilisha vyama visivyokuwa na wawakilishi bungeni, unajadili kwa undani mustakabali wa uchaguzi mkuu ujao, hali inayoashiria kwamba suala la Katiba Mpya siyo tena kipaumbele cha sasa katika siasa za nchi.
Kamati ndogo iliyoundwa na TCD chini ya Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia itawasilisha mapendekezo ya majawabu ya hoja zilizopendekezwa katika mkutano wa awali uliofanyika Agosti 31, mwaka huu katika Ikulu ya Kilimani, Dodoma na baadaye kuhitimishwa na kikao cha faragha cha viongozi wa vyama hivyo katika Hoteli ya St Gaspar.
Mbali na Mbatia wajumbe wengine ni wale wanaotoka kwenye vyama ambavyo viko kwenye mvutano kuhusu Bunge Maalumu wakiwamo wale wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa upande mmoja na CCM kwa upande mwingine.
Hao ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati CCM kinawakilishwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana ambao kwa pamoja watawasilisha mapendekezo ya kumaliza mvutano uliopo pamoja na mwafaka kuhusu namna bora ya kuendesha uchaguzi mkuu ujao.
Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata zinasema miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakisukumwa kwa nguvu na Ukawa hata walipokutana na Rais mara ya kwanza ni kusitishwa kwa Bunge Maalumu kwa maelezo kwamba Katiba Mpya siyo tena kipaumbele cha nchi na kwamba fedha zinazotumika zingeelekezwa katika mambo mengine muhimu ya nchi.
Ukawa unaoundwa na vyama vya NCCR- Mageuzi, CUF na Chadema, wajumbe wake katika Bunge Maalumu walisusia vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu kwa maelezo ya kwamba hawaridhishwi na mambo yanavyoendeshwa na baadaye kuanza kushinikiza kusitishwa kwake.
Hata hivyo, suala la kusitishwa kwa Bunge Maalumu limekuwa gumu kutokana na kutokuwapo kwa mwanya wowote wa kisheria unaomruhusu Rais Kikwete kuchukua hatua hiyo, lakini habari zinasema ‘mlango pekee uliobaki’ ni Oktoba 4, 2014 ambayo ni siku ya mwisho iliyotajwa kwenye tangazo la Serikali.
“Nadhani hata mheshimiwa Rais ameshaombwa asitoe GN (tangazo lingine) ya kuongeza siku za Bunge Maalumu kama wajumbe wa Bunge wanavyotaka, kwa hiyo kama atakubali ni dhahiri kwamba Bunge litakoma tarehe 14 mwezi ujao (Oktoba),” kilisema chanzo chetu kutoka serikalini.
Ikiwa Rais ataamua kutobadili tangazo lake, basi Bunge Maalumu litasitisha shughuli zake, kwani tayari lilishapanga ratiba inayoonyesha kuwa litaendelea hadi mwishoni mwa Oktoba wakati Mwenyekiti wake, Samuel Sitta atakapokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete.
Tarehe ya mwisho
Licha ya tarehe ya mwisho ya Bunge hilo ambayo ni Oktoba 4, 2014 kutangazwa na Rais Kikwete Julai 28 mwaka huu na kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti 1, 2014, Bunge Maalumu lilibadili kanuni zake, hatua ambayo ilitaja siku sitini zilizotolewa na Rais kwamba ni za kazi tu.
Awali katika azimio lake la Aprili 4, mwaka huu, Bunge Maalumu liliipitisha Jumamosi kuwa moja ya siku zake za kazi kwa kuongeza kipengele cha nne katika Kanuni ya 14. Sehemu ya Kanuni hiyo inasomeka: “Bunge Maalumu kwa siku za Jumamosi litakutana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana…..”.
Hata hivyo, Agosti 5, 2014 Bunge hilo lilipitisha azimio lingine ambalo lilirekebisha kanuni hiyo ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku zilizotajwa kuwa za kazi. Sitta aliwaambia wajumbe wa Bunge hilo kwamba Rais Kikwete alikuwa tayari ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazitajumuisha Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.
Baada ya mabadiliko hayo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad aliandika barua serikalini akitaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo, lakini hadi sasa barua hiyo haijajibiwa.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wiki hii aliliambia gazeti hili kwamba Rais Kikwete alikuwa amepokea maombi ya Bunge Maalumu ili arekebishe tangazo lake la awali na kwamba bado yanafanyiwa kazi huku akisisitiza kuwa uamuzi wa Rais lazima utazingatia sheria.
Sefue alitoa kauli hiyo huku akisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alikuwa sahihi katika tafsiri aliyowahi kuitoa akisema kwamba siku zinazotajwa kwenye gazeti la Serikali kwa ajili ya Bunge Maalumu ni za kikalenda na siyo za kazi kama ilivyotafsiriwa na uongozi wa Bunge hilo.
Mwanasheria katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Harold Sungusia akizungumzia suala hilo jana alisema kifungu cha 28 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ndicho kinachoelekeza jinsi nyongeza ya siku inavyopaswa kufanyika wakati kifungu cha 27 (3) cha sheria hiyo pia kinalipa Bunge Maalumu uwezo wa kutunga kanuni za jinsi ya kuendesha mambo yake.
“Sheria iko wazi na hapa tafsiri sahihi ya siku zilizoongezwa inaweza kutolewa na mahakama kwani Mwanasheria Mkuu wa Serikali hana nafasi katika Bunge hili na hapo ndipo tatizo lilipo kwamba kuna watu wanadhani kwamba hili ni Bunge la kawaida, sivyo hata kidogo,”alisema Sungusia.
Hoja ya kutaka Bunge Maalumu kusitishwa mapema kama ilivyo kwenye tangazo la Serikali inatokana na ukweli kwamba ratiba yake ya sasa inaingiliana na ratiba za vikao vya Bunge la Muungano ambalo limepangwa kuanza Novemba 4, 2014 na Baraza la Wawakilishi ambalo limepangwa kukutana kuanzia Oktoba 22 mwaka huu.
Kwa upande wa Bunge la Muungano, Katibu wake Dk Thomas Kashililah alisema kuna kamati za kisekta zinapaswa kuanza vikao vyake Oktoba 10 kwani kuna miswada mingi ya Serikali inayopaswa kufanyiwa kazi mapema.
Rais na TCD
Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo aliliambia gazeti hili mjini Dodoma siku chache zilizopita kwamba mazungumzo baina yao na mkuu huyo wa nchi yanalenga mambo muhimu ya kuwezesha kuwa na mazingira bora ya uchaguzi mkuu wa 2015 na siyo vinginevyo.
“Tuna mambo muhimu na hayo diyo tumekuwa tukizungumza, mambo ya Tume Huru ya Uchaguzi, mambo ya mgombea binafsi, kuhojiwa kwa matokeo ya urais, hayo ndiyo mambo tunayozungumza kuona jinsi gani tutaweza kuwa na mwafaka wa pamoja maana hata kama Katiba Mpya ikipitishwa leo haiwezi kutumika kwenye uchaguzi mkuu,” alisema Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa UDP.
Baada ya mkutano wa Agosti 31 mwaka huu katika Ikulu ya Kilimani, Dodoma na baadaye katika Hoteli ya St Gaspar pia ya mjini humo, viongozi wote walitoa tamko la pamoja ambalo pamoja na mambo mengine lilitaja kuundwa kwa kamati ndogo ili kuzifanyia kazi hoja kadhaa zilizowasilishwa kwenye kikao hicho.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kamati hiyo ilifanya vikao vyake jijini Dar es Salaam na leo wajumbe wake watasafiri hadi Dodoma kwa ajili ya mkutano wa awamu ya pili na Rais Kikwete.
SIMULIZI: Namna Freemason ilivyoingia Tanzania, Afrika Mashariki โ€“ 2

SIMULIZI: Namna Freemason ilivyoingia Tanzania, Afrika Mashariki – 2

Wakati ule, hata hivyo, Ofisi ya Freemason Afrika Mashariki ilikuwa imetoa mchango mkubwa katika kusaidia kuimarisha ufreemason katika sehemu za bara.
Hatua ya kwanza ya Freemason ilikuwa ni kuimarisha uchumi, biashara na shughuli za kisiasa. Baadaye nguvu ikaelekezwa zaidi eneo la bara la Afrika Mashariki, siyo kwa Wajerumani wa Afrika Mashariki, bali kwa Wakenya, ambapo kukamilika kwa ujenzi wa reli ya Uganda kulikuwa tayari kumeanza kuonyesha matokeo mazuri katika eneo kubwa lililokuwa makazi ya wazungu Afrika Mashariki.
Zanzibar ilikuwa tayari imeshapiga hatua nzuri katika masuala la kilimo, biashara na miundombinu wakati huo.
Mwaka 1901, bidhaa ya kwanza ya majani ya chai Afrika Mashariki ilitengenezwa huko Dunga.  Mwanzoni majani hayo yalilimwa kwenye bustani iliyoanzishwa mwaka 1899.  Majani yalikuwa yakitengenezwa kwa kutumua zana za mikono, kuanikwa juani na kukaangwa kwa kutumia jiko la kawaida la mkaa.
Baadaye mwaka uleule, kiwanda cha kwanza cha mafuta kilianzishwa Zanzibar kikifuatiwa na ujenzi wa tangi katika mji wa Mtakuja. Tangi hilo lililowekwa na Messrs Smith Mackenzie na kampuni yake kama wakala wa Kampuni ya usafirishaji na biashara ya Shell Ltd, lilikuwa kwa ajili ya kukusanya mafuta mengi.
Pia kampuni hiyo ilijenga kiwanda kwa ajili ya kutengeneza mapipa ya kuwekea mafuta ya taa.
Mwaka 1903, gazeti la kwanza huko Zanzibar lililojulikana kama “Samachar” lilichapishwa. Baadaye gazeti hilo lilikuwa likichapishwa kila siku, huku chapisho lake la kwanza likitoka Agosti 21, 1905. Baadaye magazeti mengi tu yalichapishwa Zanzibar.
Mwaka 1903, nyumba nzuri zilijengwa Kigomasha huko Pemba na Chumbe. Mwaka uliofuata, Freemason Kenya waliomba kupewa hati ya kutambuliwa ili waanzishe ofisi.
Ofisi hiyo Namba 3084 ilifunguliwa rasmi Mei mosi, 1905. Baadaye, ilipandishwa ngazi ya juu zaidi. Mimi ni mwanachama katika ngazi hiyo.
Sultani wa Zanzibar alisisitiza ujenzi wa miundombinu. Ufaransa walifungua ofisi ya posta iliyokuwa ikitoa stempu za aina mbalimbali baada ya kuwepo zilizotolewa na nchi hiyo kati ya mwaka 1870 na 1900.
Shule ya familia ya kifalme na Waarabu daraja la pili ilifunguliwa, huku kampuni ya Marekani ikijenga njia ya reli kuunganisha Bububu na Forodhani na baadaye kuiuzia Serikali mwaka 1911.
Mwaka 1905, nyaya za umeme zilifungwa umbali wa maili tano kuzunguka kasri la mfalme. Kazi hiyo ilifanywa na Mr J.A. Jones wa New York.
Kitu cha kuvutia, mitaa ya Zanzibar ilikuwa na umeme mapema zaidi kuliko mitaa ya London, ambako walikuwa bado wanatumia taa za gesi.
Kampuni ya Marekani ilifunga huduma ya simu katika kituo cha simu cha Old Fort na Ofisi ya Posta huko Shangani.
Hata hivyo, huduma za posta ambazo zilikuwa zimeanza mwaka 1873 katika jengo la Mackenzie zilikuwa tayari zimeunganishwa na umoja wa posta.
Reli  ya Uganda ilikuwa imeanzisha njia ya kuimarisha ukoloni zaidi katika eneo la bara. Jambo hili lilileta maendeleo na kuanzishwa kwa makazi mapya Kenya na Uganda.
Kadri ya muda ulivyokwenda, baadaye maeneo hayo yalikuja kuwa vituo muhimu vya Freemason kukua na kupanuka katika eneo lote la Afrika Mashariki.
Ofisi ya Freemason namba 3084 ilifanya kazi nzuri sana. Kazi ya kwanza ya Freemason mjini Nairobi ilikuwa kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka.
Katika kufanikisha jambo hilo, ofisi iliamua kuwapandisha ngazi wanachama wote katika mkutano mmoja jambo ambalo linazuiwa na katiba ya Freemason.
Ofisi iliweka makazi yake ndani ya jengo la Posta katika mtaa wa Victoria (siku hizi unaitwa Tom Mboya). Ilikuwa ikitumia kinanda ilichoazima kutoka Kanisa la Mtakatifu Stefano. Ofisi hiyo ikiwa chini ya mwangalizi kutoka Scotland, ambaye ofisi yake iliitwa Scotia namba 1008, ilianzishwa mwaka 1906.
Kijana mdogo mwanachama katika ofisi ya Harmony aliteuliwa kuwa mkuu wa kwanza wa ofisi ya Scotia. Kutokana na ofisi ya Harmony kuisaidia ofisi ya kwanza ya Scotland wakati wa kufanya sherehe zao, utamaduni na mambo mengine, utaratibu huo ulizoeleka kwenye mfumo mzima kiasi cha kuleta utata kwa wanachama wa Freemason kati ya ofisi hizo mbili.
Kwa miaka mingine sita, Sir Charles Bowring, ambaye alitumika kama gavana wa makazi awamu  tatu, alitoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Freemason Kenya na Uganda.  Alikuja kuteuliwa kuwa Mkuu wa kwanza wa uchaguzi kwa nchi za Afrika Mashariki.
Miaka miwili baadaye, mwaka 1909 na 1910, yalitokea mambo makubwa mawili ambayo yalionyesha ukuaji wa Freemason Afrika Mashariki. Septemba 1909, ofisi ya Harmon namba 3084 ilipewa heshima ya kutembelewa na Rais wa Marekani, Theodore Roosevelt – mwanachama wa Freemason aliyekuwa amemaliza kwa mafanikio katika muda wake wa mihula miwili kama Rais ndani ya Ikulu ya Marekani.
Roosevelt alikuwa amekuja Afrika kwa mwaliko wa Taasisi ya Smithsonian ya Washington. Ziara yake ilisherehekewa zaidi kwa kumtunuku tuzo nyingi kuliko alivyotarajia kutoka kwenye taasisi ya kitaaluma.

Kategori

Kategori