IPTL/PAP: SISI SIO SHIRIKA LA UMMA.









NA MWANDISHI WETU.

Kampuni ya IPTL/PAP imewataka wanasiasa kuzingatia ukweli halisi kuhusiana na kampuni hiyo kuwa ni kampuni binafsi inayojishughulisha na uzalishaji na uuzaji wa  umeme na si shirika la umma.

Pia, imesema kuendelea kujadili masuala ya ndani ya uendeshaji ikiwemo namna ya  kuuza na kuzalisha umeme, umiliki na uhalali wa kampuni, uuzaji na ununuaji wa hisa za kampuni ni masuala binafsi ya kampuni .
Taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari jana mjini Dar es saalam, Katibu na mshauri wa sheria wa kampuni hiyo Joseph Makandega  ilisema  IPTL/PAP ni wadau wa kuzalisha na kuuza umeme kwa shirika la umeme  nchini(TANESCO).

Ilisema kinacho waunganisha IPTL na umma ni huduma wanayo itoa kwa TANESCO ya uuzaji wa umeme, hivyo kulazimisha umma  kujadili mambo ya IPTLya sasa na  ya zamani  ni upuuzi unaopaswa kudharauliwa .

“Kulazimisha umma kujadili migogoro ya sasa nay a zamani kama mgogoro wa Mechmar na VIP ni sawa na kuwalazimisha watu wajadili migogoro mingine binafsi ya kampuni ambayo si ya umma,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo. Taarifa hiyo iliongeza; “pia ni sawa na kulazimisha jamii fulani iache shughuli zao na kujadili mambo bimafsi ya mtu, jambo ambalo si haki na ni upuuzi na inapaswa kukemewa .

Ilisema kampuni binafsi na makini kama IPTL/PAP ina sera zake na misingi yake  ya uendeshwaji , hivyo kuruhusu hisia binafsi za wanasiasa uchwara kutawala mjadala kuhusu uendeshwaji wa kampuni ni upuuzi wa kiwango kikubwa.

“Nawasihi wanasiasa hawa japo tunatambua ni wakina nani  wanawatumia na kwa maslahi gani? kamwe wasichokoze moto wasioweza na muda si mrefu tutaweka wazi uozo wao wote ,”ilisisitiza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Makandege ilisema inawashauri wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele  kueleza uongo juu ya  IPTL/PAP kuwekeza nguvu zao katika kutimiza ahadi zao walizozitoa kipindi cha uchaguzi ikiwemo kuinua uchumi wa wananchi wanao waongoza.

Alisema  miongoni mwa wanasiasa hao viherehere wameshindwa kutimiza ahadi zao na sasa wanatafuta umaarufu wakisiasa kupitia suala la  IPTL na kuaminisha  umma kuwa mali yao wakati sio kweli .

Hivyo, taarifa hiyo ilisema IPTL/PAP inajua ni namna gani hisa za VIP walivyozinunua. Vilevile inafahamu namna hisa za Mechmar zilivyo nunuliwa sisi ni wataalamu wa masuala ya biashara , uwekezaji, uzalishaji, na viwanda hii si siasa wafanye siasa yao bila kuingilia masuala ya kitaalamu. Kupoteza muda wa watanzania kuwajadilisha masuala binafsi tena kwa uongo wa hali ya juu ni jambo ambalo halivumiliki kuwakalia kimya wanasiasa  kwahivyo ni kuutumia vibaya muda wa watanzania.

Makandege aliwakaribisha watanzania wote wanaotaka kufahamu maswala mbalimbali yanayohusiana na IPTL/PAP ikiwemo umiliki na uzalishaji wa umeme  kutafuta taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi  ambavyo ni wao na si wanasiasa.


Yapo masuala, taasisi na mashirika ambayo ni mali ya umma na watanzania wanaona namna ambavyo yanafujwa na mengineyo yanafujwa na wanasiasa haohao waliojivika usemaji wa IPTL,huku wakishinwa kuyatetea mashirika hayo na badalka yake wamekuwa sehemu ya ufujaji na wanaifanya IPTL kama kivhwa cha kujifichia tunaushahidi na vielelezo vyote na tutaweka wazi muda wowote ili watanzania wawapime malaika hao kama ni malaika au mashetani.

SOURCE: GAZETI LA MAJIRA

7 comments

hii kweli kabisa hawa wakina kafulila hawaoni makampuni ya umma yanavyofujwa wao wameng'ang'ania kampuni binafsi,wanataka nini hawa au rushwa

Hivi hawa mbwa kina KAFULILA na ZITTO KABWE wanamtatizo gani mbwa hawa?? Wamekaa kama mademu mbwa hawa kazi kupika majungu tu wanashindwa kutekeleza ahadi walizozitoa majimboni kwao mbwa hawa wanabaki kufanya majungu mjini hapa!! wataliwa mbwa hawa

Hakuna haja ya kuwaficha hawa ni Mbunge DAVID KAFILILA na ZITTO KABWE. Wanasiasa uchwara hawa, wachumia tumbo. Kazi yao ni kutengeneza scandal ili wapate riziki.Kwa IPTL/PAP wamechemsha, watapiga kelele mpaka makoo yawakauke. Watanzania tumegundua hila zao.

n times like this haya mambo ya mascandal yatasikika sana as long as mwakani ni uchaguzi yatakuwa yaleyale kama 2010, leo tumepata wabunge wa scandal ya EPA/RICHMONDS walipita hivihivi baada ya watanzania kuhemka. Ndio leo tunao kina KAFULILA na wengineo, wameshindwa kutekeleza ahadi zao wamebaki kubeba fitna na migogoro ya kibiashara ya watu wengine.

Bongo kuna wanasiasa basi, wachumia tumbo tu hawa jamaa, nakumbuka KAFULILA na familia yake walivyo kuwa wakicheza ngoma yakwao pale bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge. Mpaka kichefuchefu

PAP/IPTL wapuuze hizi mbwembwe za wanasiasa wao waconcetrate kwenye kuhakikisha wanatugea umeme watanzania kama walivyoahidi kwenye mikataba yao

mpaka kielewekeeeeee!!!!


EmoticonEmoticon