MWANAMKE AUAWA NA TEMBO

 

 


Chris Bomola

Tembo hao ni wa kutoka hifadhi ya Lwafi

Mwanamke wa miaka 60, ameuawa na tembo katika Wilaya ya Kalambo iliyoko Magharibi mwa Tanzania.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema, tukio hilo lilitokea wakati marehemu akiwa anarejea kutoka shambani kwake majira ya saa nne asubuhi.
Hifadhi ya Lwafi inapatikana pembezoni mwa barabara ya kutoka Tanzania kuelekea Zambia.
Akithibitisha kutokea tukio hilo Mkuiu wa Wilaya ya kalambo Bi Julieth Binyura amewataka wananchi kuacha kuwafukuza tembo wanapoingia katika maeneo hayo badala yake kusubiri wataalamu kufanya kazi hiyo.

RAMAPHOSA: HAKUNA KINGA YA RAISI ZUMA DHIDI YA MASHITAKA YANAYOMKABILI



Raisi wa Chama cha ANC Cyril Ramaphosa ameiambia Kamati Kuu ya Chama hicho kuwa  Hakuna kinga dhidi ya mashitaka yanayomkabili Raisi wa nchi ya Afrika Kusini Bwana Jackob Zuma.Na sio moja ya makubaliano katika kukabidhiana madaraka.
Chanzo: News24

KUTANA NA HARMONY MDOLI WA NGONO ANAYEONGEA



Mageuzi ya teknolojia yamesababisha mabadiliko mbalimbali katika njia za binadamu, Kwa siku za karibuni kumekua na ongezeko kubwa la uzalishaji wa Midoli ya ngono, ambayo inasemekana mahitaji yake kwa sasa yameongezeka.
Harmony ni moja ya zao la mageuzi ya midoli ya ngono, mdoli Harmony anaweza kuongea na kutembea kwa kutumia teknolojia ya robot iliyotumika kumtengeneza.

SERIKALI KUJENGA ''FLYOVER'' NYINGINE SABA



Serikali katika kukabiliana na tatizo la foleni za barabarani imepanga kujenga vivuko saba vya juu vya barabara (flyover)
hayo yamesemwa na Msemaji wa Serikali Dr Hassan Abbas wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Barabara zitakazohusika na ujenzi wa flyover hizo ni Chang'ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni na Tabata.

WAKILI WA UPINZANI KENYA ATIMULIWA



Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake
Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna
Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009.
"Kwa mantiki hiyo hati ya kusafiria ya Kenya ya bwana Miguna ilikuwa na bado ni batili", alifafanua bwana Njoka
Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baada ya kushiriki katika kiapo kisicho rasmi cha Raila Odinga kuwa rais wa watu wa Kenya mwezi uliopita.
CHANZO: BBC SWAHILI

Kategori

Kategori