SHAHIDI: SIAJONA BALENGA AKIMUUZIA NYUMBA MACHA.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana ilisikiliza ushahidi wa mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Hans Aingaya Macha akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili ya kughushi.
Macha alitoa ushahidi wake, wakati upande wa mshitakiwa unaoongozwa na Wakili Deogratius Ringia mbele ya Hakimu Devotha Kisoka mahakama hapo jana.
Mfanyabiashara huyo, alidai mahakamani hapo kuwa nyumba ya ghorofa tano kilichopo katika kiwanja namba 183 ‘A’ kilichopo Kigogo, aliinunua kwa Ramadhan Balenga huku akiwa pia anamdai Balenga.
Hata hivyo, Wakili wa serikali Nassoro Katuga alipomuuliza swali mshitakiwa huyo aonyeshe ushahidi wake, ikiwemo nyaraka za madeni na awataje majina ya mashahidi waliokuwepo wakati akinunua nyumba hiyo ya ghorofa tano kwa sh. Milioni 20, alidai wapo.
Kitendo ambacho, kilimfanya mshitakiwa huyo kudai mahakamani hapo kwa jina moja tu, ndipo aliwapowaambia awataje na yeye aliwataja akiwemo mfanyakazi wa Balega aitwaye Mohammed Waziri.
Alipomaliza kutoa ushahidi wake, Macha, ndipo zamu ya Wazir ilifika, ambaye alidai mahakamani hapo kuwa hakuwahi kushuhudia mauzo yeyote yakifanyika kwa kuwa wakati huo alishaondolewa katika biashara alizokuwa akizifanya.
“Sifahamu chochote kuhusiana na Balenga kuuza nyumba, ingawa niliambiwa na watu wa pembeni, akiwemo Macha mwenyewe, hivyo huo ndio ukweli wenyewe Mheshimiwa Hakimu ninaoujia,’’kauli ambayo iliamsha cheko katika chumba cha mahakama kutokana na ushahidi wake huo.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa mke wa Balenga, Nully Ahmady alidai mahakamani hapo kuwa hata yeye hakushuhudia wakati akiuza nyumba hiyo, kwa kuwa alikuwa tayari ameshaachana naye. Kesi hiyo inaendelea tena mahakamani hapo.

 Picha: Mfanyabiashara Macha

SOURCE: Jamii Forums.


EmoticonEmoticon