SIMBA MTANI JEMBE WA UKWELI

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Akiuwahi mpira wa uliokuwa umetemwa na golikipa wa Yanga SC, Deogratius Munish ‘ Dida’ ambaye alishindwa ‘ kiki ya umbali wa mita zipatazo 23’ ( adhabu ndogo) iliyokuwa imepigwa na mchezaji aliyekuwa bora zaidi katika mchezo huo baina ya mahasimu wa kandanda nchini, Yanga SC na Simba SC uliofanyika katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Emmanuel Okwi ambaye alivaa beji ya unahodha kwa mara ya kwanza kwa upande wa Simba alipiga mpira ambao ulitemwa na Deo kisha kiungo, Awadh Juma akafunga bao la kuonga kwa timu yake katika dakika ya 30.
Dakika tatu kabla ya muda wa mapumziko mshambulizi Elius Maguli akafunga bao lingine akimalizika mpira uliokuwa unarudi uwanjani baada ya kugonga mwamba kufuatia ‘ kiki’ ya kiungo, Mganda, Simon Sserunkuma. Mabao hayo mawili yalisimama hadi mwisho wa mchezo na kwa mara ya pili mfululizo ‘ Wekundu wa Msimbazi’ wanatwaa ushindi wa ‘ Nani Mtani Jembe-2’. Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita, Yanga ilipoteza kwa mabao 3-1.
MARCIO MAXIMO…….
Wakati Fulani katika kipindi cha pili kocha huyo wa Yanga alionekana ‘ akijaribu kufunga na mchezaji wake’. Nilimshangaa zaidi pale alipojaribu ‘ kuhitaji huduma ya mchezaji alikwisha choka’. Maximo alikuwa ni mwenye presha kubwa na alitamani walau kuona timu yake ikifunga bao dhidi ya Simba lakini hakuwa na mbinu bora.
Patrick Phiri amecheza mchezo wa 12 dhidi ya Yanga akiwa kocha wa Simba, amepoteza mara moja tu na kwenda sare mara tano, ushindi mara sita bila shaka ‘ unaweza kumuita kiboko ya makocha wa Yanga’, ilikuwa ngumu kwa Yanga kushinda kutokana na mfumo mgumu wa kiuchezaji walioingia nao, pia uchaguzi wa wachezaji haukuwa bora.
Mbuyu Twite, Emerson Oliveira, Haruna Niyonzima, Saimon Msuva na Andrey Coutinho walianza katika eneo la kiungo wakiwa wachezaji watano ambao mbele yao alisimama mshambulizi, Kpah Sherman. Yanga walianza vizuri mchezo huo, walicheza kwa kupasiana huku wakiwa na hali ya kujiamini. Wingi wa wachezaji wao katika eneo la kiungo kulifanya waonekane ni timu imara zaidi, lakini hali hiyo ilitoweka baada ya Simba kuanza kuwabana na kucheza pia kwa kujiamini.
Tukio la Kelvi Yondan la kumfanyia madhambi Emmanuel Okwi katika dakika 15 liliongeza presha kwa Yanga, inawezekana mwamuzi ‘ Mwanamama’ Jonesia Rukyaa alichemsha kutokana na kutofuatilia kwa makini tukio hilo la Kelvin kumchezea faulo Okwi pasipo kuwa na mpira. Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Niyonzima mara kwa mara walikuwa wakimzonga mwamuzi. Awadh, Jonas Mkude na Sserunkuma wakaanza kutawala kiungo, na nguvu ile na stamina walizokuwa nazo wachezaji wa Yanga katika robo saa ya kwanza ya mchezo zikatoweka. Mawasiliano kati ya safu ya kiungo na ile ya mshambulizi ‘ yakafa’, wakakubali kusogezwa nyuma ya lango lao na Simba wakamaliza mechi kwa stahili ya ‘ rebound’ mipira iliyorudi kutoka katika goli la Yanga.
Katika muda wa dakika 90, Maximo alitumia washambualiaji wanne, Sherman aliyeanza kama mshambulizi huru, kabla ya Danny Mrwanda kuingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Coutinho ambaye hakufanya lolote katika mfumo wa awali wa 5-4-1. Alipoingia Mrwanda angalau hata Maximo mwenyewe aliona dalili za kupata bao lakini alikwisha chelewa, Phiri alimmaliza na wachezaji waliouchezesha ‘ sawia’ mfumo wa 4-3-3.
Kwa mara ya pili, Yanga chini ya Maximo imeshindwa kupata goli dhidi ya Simba, lakini baada ya suluhu-tasa, mwezi Oktoba katika mchezo wa ligi kuu, Phiri alishajua namna ya kuishinda Yanga. Ni kuwawkea mshambulizi msumbufu na mwenye nguvu walinzi ‘ wenye jabza’ Nadir Haroub na Kelvin.
Maguli alikuwa bize kukimbia na mipira, haijalishi mara ngapi aliicha nyuma, lakini kila aliposogea katika eneo la hatari la Yanga alikuwa mwenywe nguvu. Tuwe wa kweli, Yanga inahitaji mlinzi wa Kimataifa labda ndiyo wataweza kushindana barani Afrika hapo mwakani.
Kelvin anahitaji kujitazama upya, amekuwa ni mchezaji mwenye hasira za haraka huku matukio yake yakiwa ya wazi. Alikimbizwa hasa na alionekana kuchoshwa na washambuaji watatu wa Simba waliokuwa wakihamahama, nawazungumzia Okwi, Maguli na Ramadhani Singano. Kitu cha kujivunia kwa Yanga ni uwepo wa kiongozi wa kweli, nahodha, Nadir, Kelvin anaweza kujifuna mengi kutoka wa ‘ patna wake huyo’ ili kuifanya Yanga kuwa bora.
max
Maximo alianza na wachezaji wote wa kigeni, lakini chaguo la kuwaazisha nje, Dilunga, Ngassa na Mrwanda na kuwaanzisha, Coutinho, Sherman ambaye alitua nchini siku mbili kabla ya mchezo huo hakika halikuwa chaguo bora na amevuna alichopanda.
Sserunkuma alicheza kwa mara ya kwanza, aliipandisha timu kwa kasi mara nyingi hasa baada ya Simba kutawala mchezo, alikimbia na mipira huku akigawa pasi zilizofika kwa walengwa, juhudu zake zilizaa bao la pili kwa timu yake baada ya kusogea na mpira na kupiga kiki ya umbali iliyogonga mwamba na kumkuta mfungaji katika dakika ya 42.
Mganda huyo anayeichezea Express alicheza kwa dakika 84 na kumpisha Shaaban Kisiga anaisaidia sana Simba ambao wanahaha kupata kiungo mwenye kupandisha timu kwa kasi huku akipiga pasi za uhakika. Alimpunguzia majuku mengi Mkude, na alitawala ‘ duara’ akishirikiana na Awadh. Nahodha, Joseph Owino alianzia katika benchi kumpisha, Mganda, Juuko Murushid kucheza na chipukizi, Hassan Isihaka.
Nassoro Chollo alianza katika nafasi ya ulinzi wa kulia alipoteza mipira mingi huku akipiga pasi za hovyo mara kadhaa, alicheza dakika zote 90 lakini bado anahitaji kujiimarisha zaidi na kupunguza papara anapokuwa na mpira. Mohhammed Hussein aliendelea kuwa na kiwango bora, alianza katika beki tatu na aliimarisha ukuta wa Simba.
SIMBA SC, IVO Mapunda, Nassoro CHOLL, Mohamed Hussein ‘ TSHABALALA’/ Issa Rashid ‘ BABA UBAYA’ dk 66, Hassan ISIHAKA, Juuko MURUSHID/ Joseph OWINO dk 47, Jonas MKUDE, Ramadhani SINGANO/ Said NDEMLA dk 74, AWADH Juma, Elius MAGULI/ Danny SSERUNKUMA dk 84, Simon SSERUNKUMA/ Shaaban KISIGA dk 84, Emmanuel OKWI.
YANGA SC, Deogratius MUNISH, Juma ABDUL/ Hussein JAVU dk 79, Oscar JOSHUA, Nadir HAROUB, Kelvin YONDAN, MBUTU Twite/ Hassan DILUNGA dk 39, EMERSON Oliveira/ Salum TELELA dk 55, Haruna NIYONZIMA, Kpah SHERMAN/ Mrisho NGASSA dk 63, Saimon MSUVA, Andrey COUTINHO/ Danny Mrwanda dk 46…
0714 08 43 08
habari kwa hisani ya Shaffii Dauda Blog





EmoticonEmoticon